Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

Wednesday, September 17, 2014

MFANYABIASHARA MAARUFU ACHINJWA NA KUTUPWA KICHAKANI

Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.


 Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam ameuawa kwa kuchinjwa na watu  wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.


Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike  katika eneo  hilo mwaka 2005.


Mke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani),  alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti.


Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo  hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lusu wilayani  Nzega, Mkoa wa  Tabora  walielekezwa  kwa  marehemu huyo.


Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika  nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la hekari tatu


Mke huyo alisema hata yeye tukio hilo limemchanganya kwani aliamini wale vijana walikuwa ni watafutaji na ndiyo maana mumewe aliwapa shamba, kumbe walikuja kutafuta roho ya mume wake.


Alisema tangu watu hao wafike, siku tatu mbele ndipo walipogundua mumewe amechinjwa na vijana hao watatu hawajaonekana tena. 


Alisema siku ya tukio, mume wake aliondoka na vijana hao kwa madai wanakwenda kumtolea pesa kwenye mtandao wa simu ili wamlipe kwa ajili ya shamba hilo.


Kwa mujibu wa Rehema, watoto wake wawili (mmoja miaka 7, mwingine 4) ndiyo waliogundua mwili wa marehemu baba yao akiwa amechinjwa walipokwenda kuchunga ng’ombe.


 “Nikiwa bado najiuliza aliko mume wangu, mara mtoto wangu Ashura (mkubwa) akaja anakimbia huku ana wasiwasi, akasema, mama nimeona shati la baba, ndala na mguu wake. Ndipo tukaenda huko na watu lakini Ashura  alikataa kufika kwa awamu nyingine.


“Tulipofika tuliukuta mwili wa mume wangu. Niliona amekatwa kichwani na pembeni kulikuwa na panga. Baada ya hapo nilihisi mwili ukiishiwa nguvu, sikujua nini kilichoendelea,” alisema mwanamke huyo.


Mpaka sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke linawashikilia  watu watatu, wawili wakiwa ni wale waliowakaribisha wale vijana huku mmoja wao akiwa mwenyeji wa kijiji cha jirani, alikamatwa kutokana na maelezo ya bahasha iliyokutwa kando ya mwili wa marehemu ikisema ‘kumbuka yaliyotokea mwaka 2013’ ambapo baadhi ya watu walisema mtuhumiwa huyo aliwahi kutofautiana na marehemu.


via>>africanmishe blog
Read More >>

Tuesday, September 9, 2014

Picha 3 za kituo cha Polisi kilichovamiwa Geita alafu Polisi wawili wakauliwa na watu wenye silaha.


Geita Polisi 2014 2 
Nilisoma moja ya gazeti lililokua limeandikwa IGP atangaza dau la milioni 10 kwa yeyote atakaefichua wanaohusika na uvamizi wa kituo cha Polisi ambao pia walifanya mauaji ya Polisi wake wawili Bukombe Geita.
Geita Polisi 2014 3 
Baadhi ya mashuhuda wamekubali kuzungumza na  akiwemo mlinzi ambae anafanya kazi eneo jirani na kituo hiki anaesema ‘Ilikua kitu kama saa tisa na dakika 40 niliona magari yanapitapita pamoja na pikipiki, kama muda wa dakika 5 nikasikia kitu kama tairi kimepasuka hisia yangu kwavile ni mlinzi mzoefu nilishtuka nikasema mbona hilo sio tairi manake gari sikuiona, kidogo tena nikasikia mengine yanapigwa kama mara tatu’
‘Vibunduki vidogo vikawa vinapigwa chapchap tu nikaanza kushangaa na kuanza kujifichaficha kukimbia huku na huku, ilipofika saa mbili tukakuta watu wawili wameuwawa Mwanamke mmoja na Mwanaume mmoja wametupwa kwenye mtaro barabarani, matukio kama haya yameshajitokeza mengi tu Geita mwingine amenyongwa tu barabarani lakini tuna muda mrefu hatukuyaona/kuyasikia’

Geita Polisi 2014 1Shuhuda Mwanamke ambae anaeishi karibu na eneo hili anasema alikua amelala wakati tukio linatokea na alilisikia, anachoomba ni idadi ya Polisi kuongezwa kituoni hapo ili kuongeza nguvu zaidi hata 100 akisema ‘kile kituo ni kikubwa lakini askari ni wachache’
Wakati tukisubiria ripoti nyingine ya Polisi kuhusu hili tukio unaweza kuwasikiliza mashuhuda wenyewe hapa chini.

Chanzo: millardayo.com
Read More >>

Saturday, September 6, 2014

Majambazi yavamia kituo cha polisi yapora silaha na kuua wilaya ya Bukombe.

Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi wilaya ya bukombe na kuua askali polisi wawili na kujeruhi askali wengine wawili.
 
Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa jeshi la polisi Igp Ernest Mangu amesema majambazi hao walivamia kituoni hapo saa nane usiku ambapo walirusha mabomu na kuua askali wawili, waliouwawa ni  wp 7106 Uria Mwandiga  na g 2615 Dastani Kimati waliojeruhiwa ni h627 Mohamedi Hassani na cpl 5131 David  Ngupama.
 
Igp Mangu amesema katika uvamizi huo silaha mbalimbali zimeibiwa ambapo jeshi la polisi limetangaza zawadi ya shilingi millioni kumi kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao na silaha zilizoibiwa.
 
Akithibitisha kupokelewa kwa majeruhi na miili ya marehemu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe daktari Honaratha Rutatinsibwa amesema hali za majeruhi ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya rufaa Bugando.
Read More >>

Watu 36 wamefariki 79 wajeruhiwa kaitka ajali Musoma.

 

Watu 36 wamefariki dunia papohapo na wengine 79 kujerihiwa vibaya  katika  ajali  mbaya  ambayo imetokea  saa tano leo asbuhi katika kijiji cha sabasaba nje kidogo ya mji wa musoma  wilaya  ya butiama  mkoani mara  kwa kuhusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo aina ya Nissani Tellono  yenye  namba  za usajili T332 AKK.
Mbali na gari hilo kugongwa na kutumbukia ndani ya mto mmoja katika daraja hilo kwenye barabara  kuu ya Musoma –Mwanza  pia mabasi  mawili  ambayo  yamehusika  katika  ajali  mbaya ni  j4 express  yenye namba za usali  T677 CYC liyokuwa ikitokea jijini Mwanza kwenda sirari  wilayani  tarime   ambalo  limegongano  uso  kwa uso  na  basi  la  Mwanza coach yenye namba T736 AWJ lilokuwa likitokea  Musoma kwenda jijini Mwanza.
Baada ya taarifa za ajali kusambaa katika manipaa ya  musoma  vilio na  simanzi  vimetawala  katika  mji huo wa Musoma mkoani Mara  baada majeruhi  na miili ya  marehemu  wa  ajali  hiyo  kuanza kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma.
Wakizungumza wakati  wakipatiwa matibabu  baadhi  ya  majeruhi  wa ajali hiyo   wamesema  kuwa  ajali hiyo imesababishwa  na  mwendo  kasi  wa mabasi   hayo  hatua ambayo ilisababisha kushindwa kupishana katika daraja hilo hivyo  kugongana uso kwa uso.
 akizungumza  kwa niaba  ya  mganga mkuu  wa  mkoa wa  Mara Dk Martin Khan,amesema  kuwa wamepokea maiti na idadi kubwa ya majeruhi  na wengi  wao hali  zao si za kuridhisha.
Hata hivyo  Dk  Khan  ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujitolea damu kwani amesema kuwa hospital  hiyo  ya  rufaa  ya  mkoa wa  mara inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu katika kuhudimia wagonjwa wakiwemo majeruhi wa ajali.
kamanda wa polisi mkoa wa  Mara ACP Alex Kalangi, akizungumza na ITV kwa njia  ya simu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba taarifa rasmi za jeshi la polisi zitatolewa baada ya kupata taarifa  kutoka kwa madaktari na  kwamba ametoa wito kwa  wananchi kujitokea katika hospitali ya mkoa  kwaajili ya kutambua miili ya marehemu.
Read More >>

Rais Kikwete atoa nishani kwa wanajeshi 59 wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania.

Amiri jeshi mkuu rais Jakaya Kikwete ametoa nishani kwa askari hamsini na tisa wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania wakiwemo askari wastaafu waliyofariki dunia na waliyopo kazini wakiongozwa na mkuu wa majeshi jenerali Davis Mwamnyange.
Katika tukio hilo lilifanyika kwenye chuo cha maafisa wa jeshi Monduli rais Kikwete alianza kwa kuwavavisha nishani mkuu wa majeshi jenerali Davis Mwamnyange na mnadhimu mkuu wa jeshi luteni jenerali Samweli Ndomba.
 
Wakizungumza baada ya kutunukiwa nishani hizo zikiwemo nishani za operasheni safisha msumbiji na nishani ya kumbukumu ya miaka hamsini ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania askari wastafu akiwemo brigedia jenerali Hasani Ngwilizi amesema askari wastaafu wamefarijika kuona jeshi bado linawajali na waliyopo kazini wasema nishani hizo zimewaongezea ari ya kutekeleza majukumu yao katika jeshi huku wawakilishi wa askari waliyofariki dunia wakiitaka serikali iendelee na utamaduni wa kuzikumbuka familia za watu waliyotoa mchango mkubwa kwa taifa. 
 
Tukio hilo pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Alli Hasani Mwinyi waziri mkuu Mizengo Pinda mawaziri wakuu wastafu Edward Lowasa na mzee John Malechela pamoja na mawaziri wa serikali ya awamu ya nne.

Chanzo - IPP Media
 
Read More >>

Monday, August 18, 2014

SERIKALI YAJIZAJITITI KUSIMAMIA HAKI ZA MTOTO NA MAREKEBISHO YA TABIA.

 SAM_0080Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Steven Gumbo (kushoto) akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia haki za mtoto na marekebisho ya tabia leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. 
SAM_0131Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Nsachris Mwamwaja (kulia) akikanusha taarifa zilizo ripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuhusu uwepo wa wagonjwa wa Ebola pamoja na hatua za tahadhari zilizochukuliwa na serikali ikiwemo kupeleka vifaa tiba kote nchini.Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Daniel Masunzu
SAM_0073
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Frank Mvungi)
Na Frank Mvungi
Serikali imejizatiti katika kutekeleza mpango wa majaribio wa marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria katika jamii.
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bw. Steven Gumbo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
 
 “Serikali imefanikiwa kukamilisha kanuni za mahabusu za watoto, makao ya watoto na shule ya maadilisho” alisema Gumbo.
 
Pia hatua nyingine ni kukamilika kwa miongozo ya utoaji wa huduma katika mahabusu za watoto na shule ya maadilisho.
 
Hatua nyingine ni kuwepo kwa mwongozo wa  kijamiii (CRP)  wa Marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria.
 
Mafanikio mengine ni kuwajengea uwezo watumishi wote wa mahabusi za watoto na shule ya maadilisho juu miongozo mbalimbali iliyotolewa ya kuboresha huduma katika Taasisi hizo.
Akieleza zaidi Gumbo amesema kwa mujibu wa sheria ya mtoto, wanaokinzana na sheria na ambao hawajapata dhamana kutoka katika mahakama wanapaswa kupelekwa katika mahabusi za watoto, pale ambapo mahakama imejiridhisha kuwa mtoto huyo ametenda kosa huamuru apelekwe katika shule ya maadilisho.
Wizara ya Afya kupitia idara ya Ustawi wa jamii imekuwa ikishirikiana na wadau mblimbali kama vile Polisi, Mahakama, Magereza, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake.
 
Watoto wanaokinzana na sheria wanatunzwa katika mahabusi tano za watoto zilizopo katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Dar es salaam na katika shule ya maadilisho ya Irambo-Mbeya.
Read More >>

PINDA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA BARABARA WA TAMISEMI

PG4A2053
 Waziri Mkuu. Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu , Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI,  Jumanne Sajini baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro August 17, 2014 na  atafungua  Mkutano wa  Wadau wa  barabara wa Serikali za Mitaa  kwenye hoteli ya Ngurdoto Arusha August 18, 2014.  Katikati ni Waziri wa TAMISEMI , Hawa Ghasia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A2203Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Barabara  wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye hoteli ya Ngurdoti, Arusha August 18, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu PG4A2296Wazirii Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Thabiti Mwambugu wa Ruvuma (kushoto),Joseph Simbakaria wa Mtwara (wapili kusho) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Hawa Ghasia baada ya kufungua mkutano wa wadau wa barabara wa Serikali za Mitaa kwenye hoteli ya Ngurdoto ,Arusha August 18, 2014
Read More >>

WAZIRI GAUDENSIA KABAKA AIPONGEZA TPB KUTOA MIKOPO KWA WASTAAFU

Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ameipongeza Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kuandaa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF ikiwa ni fursa itakayowainua kiuchumi wastaafu hao.
Waziri Kabaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa rasmi mpango wa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF, mpango utakaowawezesha wastaafu sasa kuchukua mikopo na kuendelea kukidhi maitaji yao kipindi hicho. Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Waziri Kabaka alisema Benki ya Posta na Mfuko wa Penseni wa LAPF hauna budi kupongezwa kwa hatua ya kulikumbuka kundi la wastaafu ambalo kimikopo lilikuwa limesahaulika.
“…Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru Benki ya Posta Tanzania pamoja na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa kubuni mpango huu maalum wa kuwasaidia wastaafu kimaisha na kuwawezesha kumudu gharama za mahitaji yao na kukabiliana na ukosefu wa muda mfupi wa fedha wanazohitaji kwa kuwapatia mikopo,” alisema Waziri Kabaka.
Aliongeza kuwa mpango huo utawasaidia wastaafu kipindi cha maisha yao mapya ya kustaafu kwani licha ya muda huo wengi kuwa na kipato kidogo cha mapato lakini gharama za maisha kwao hazipungui na badala yake huendelea kupanda, jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwao.
“…Ninafarijika kuona kwamba Benki ya Posta pamoja na LAPF mmeliona hili na kulifanyia kazi, na hatimaye kuja na huduma hii ya mikopo. Lengo mahususi la mpango huu ambao kwa kiasi fulani umeanza kutekelezwa ni kuwapa faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali, ili kuweza kuboresha maisha yao na maslahi kwa ujumla,” alisema waziri huyo.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla hiyo, alisema mkopo huo ni wa kwanza na wa aina yake katika soko la mabenki nchini hivyo wanaamini utatoa hauweni kwa wastaafu wa LAPF.
Akifafanua zaidi alisema mstaafu anayehitaji kuwa na dhamana huku riba inayotozwa kwa mkopo huo kuwa ni ndogo yaani asilimia 12 tu kwa mwaka ukilinganisha na mikopo mingine. “…Mkopo huu umewekewa bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea kudaiwa. Hivyo wastaafu wote wa mfuko wa LAPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu,” alisema Moshingi.
Alisema huduma za mikopo hiyo ni za haraka na bora na zitatolewa kwa matawi yote ya Benki ya Posta Tanzania hivyo kuwataka wahitaji wote wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF kwenda katika matawi hayo popote nchini kupata maelezo ya nini cha kufanya kabla ya kupata mkopo huo.
Hata hivyo TPB kwa kushirikiana na LAPF wamezishauri taasisi za fedha nyingine zikiwemo Benki kuangalia namna ya kuweka mipango ya kusaidia wastaafu nchini kwani kundi hilo lina kiasi kikubwa cha fedha ambacho kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchango mkubwa katika uchumi wan chi ya Tanzania. Hafla hiyo pia iliyohudhuriwa na viongozi waandamizi na wafanyakazi wa TPB na Mfumo wa Penseni wa LAPF ilishirikisha pia baadhi ya wastaafu ambao baadhi walieleza wameanza kunufaika na mpango huo wa mikopo kwa wastaafu.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Read More >>

Sunday, April 20, 2014

Ukawa ruksa kufanya mikutano nchi nzima

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ruksa kwa wanachama wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya mikutano yao nchi nzima. Pinda alizungumza jana wakati akifunga maonyesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, alisema yaliyotokea bungeni yanaweza kumalizika kwa kukaa meza moja ya majadiliano.“Yale mambo ya bungeni yanaweza kumalizika na tukaendelea kama ambavyo ilikuwa katika majadiliano ya kutengeneza kanuni. Tulikuwa
tukishindana kwa kukaa meza moja na kumalizana, kisha tunaendelea sasa hili tumeshindwa nini?” alihoji Pinda Alisema: “Walitoka bungeni na kusema watazunguka nchi nzima, nasema wazunguke tu kuwaeleza wananchi na sisi hatutashindwa kuzunguka kwani hoja tunazo.Waziri Mkuu Pinda alitumia nafasi hiyo kuelezea kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwenye Kanisa la Methodist kwamba hoja ya serikali tatu ikipita inaweza kulifanya jeshi kuchukua madaraka.Alisema nilimpigia simu nikamweleza: “Rudi mara moja ueleze kilichotokea huko na nafikiri mlimsikia alichokisema.”Lukuvi akitoa ufafanuzi bungeni bila ya kuwapo kwa Ukawa alisema: “Nayasema yote haya kwa kuwa naamini huo ndio msimamo wangu na utakuwa msimamo ambao wakati wote utaendelea kuwa hivyo na ninawataka ndugu zangu kuacha unafiki.”Kutokana na kauli hizo, Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP na NCCR-Mageuzi na wajumbe 25 kutoka kundi la 201 walitoka bungeni Jumatano wiki hii na kuahidi kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kuwaleza wananchi kilichotokea.chanzo mwananchi

Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...