Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Showing posts with label matukio picha. Show all posts
Showing posts with label matukio picha. Show all posts

Monday, February 10, 2014

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah akiwasili kwa boti katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Kigoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe Bibi. Noelia Myonga, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmoud Mgimwa,Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Abdulkarim Shah na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bibi. Hadija Nyembo.
 Katikati ya Msitu wa Gombe Wajumbe wa Kamati wakipumzika kwa muda wakiwa njiani kuelekea katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe huku wakimsikiliza Mkuu wa Hifadhi Bibi Noelia Myonga (kushoto).
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Abdulkarim Shah akiwaongoza wenzake kuelekea katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe katika Hifadhi ya Gombe.
 Wajumbe wa Kamati wakiwa katika picha na baadhi ya watumishi katika Maporomoko ya Maji ya Kakombe.
 Baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati wakati wa kuagana mara baada ya kumaliza ziara yao hifadhini.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kagongo wilayani Kigoma madarasa manne yaliyojengwa na Hifadhi za Taifa kupitia Hifadhi ya Gombe.
 Madarasa manne katika Shule ya Sekondari ya Kagongo wilayani Kigoma yaliyojengwa na Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Read More >>

Wednesday, January 15, 2014

MAGARI MAWILI YAWAKA MOTO IRINGA WAKATI WANAFUNZI WAKIJIFUNZA KUUNGA NGAO


Wananchi Iringa  mjini  wakilitazama daladala  lililowaka  moto wakati likiwa kwa mafundi kuunga likichomelewa leo eneo la uwanja wa  samora
Daladala  likiwaka  moto  huku kikosi cha zimamoto na uokoaji  wakizima moto huo
Gari la Zimamoto na uokoaji mjini Iringa likizima moto  uliokuwa ukiteketeza daladala eneo la Samora  leo
Read More >>

NYUMBA ZAIDI YA 20 ZABOMOLEWA KITONGOJI CHA LUKONDE KIJIJI CHA KIKUNDA MOROGORO, WANANCHI WAKOSA SEHEMU YA KUISHI.


Nyumba ya mkazi wa kitongoji cha Lukondo katika kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka, Fikiri Buma ikiwa imebomolewa na kile kilichodaiwa kuwa ni utekelezaji wa amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya Morogoro Vijijini ambapo zaidi ya nyumba 20 zilibomolewa januari 10 mwaka huu tarafa ya Mkuyuni mkoani Morogoro.
Mkazi wa kitongoji cha Lukondo kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka Harouna Chunga (87) akiowaonyesha waandishi wa habari wa kituo cha luninga cha ITV, Sifuni Mshana mwenye kamera na Michael Msillo bendera ya CCM tawi la kitongoji hicho namna ilivyochanwa na watu wanaodaiwa kiutekeleza amri ya kubomoa nyumba katika eneo hilo januari 10 ambapo jumla ya nyumba 25 zilibomolewa mkoani Morogoro.




Mwenyekiti wa kitongoji cha Lukondo kijiji cha Kikundi kata ya Kiroka Hamdan Chawila kulia na mmiliki wa nyumba iliyobomolewa Amina Said (50) kushoto wakiangalia uhalibifu baada ya nyumba zaidi ya 20 kubomolewa na kile kilichodaiwa kuwa ni utekelezaji wa amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya Morogoro Vijijini ambapo zaidi ya nyumba 20 zilibomolewa januari 10 mwaka huu tarafa ya Mkuyuni mkoani Morogoro.


 

Na Mtanda Blog, Morogoro.
WANANCHI zaidi ya 3,00 wa kitongoji cha Lukonde kijiji cha Kikundi hawana sehemu ya kuishi baada ya nyumba zao kudaiwa kubomolewa na askari wa jeshi la polisi ikishirikiana na mgambo kwa madai ya kutekeleza amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya wilaya ya Morogoro ili kupisha ujenzi wa majosho ya kuogeshea mifugo ya mwekezaji katika tarafa ya Mkuyuni mkoani hapa.

Katika tukio hilo lililotokea januari 10 kuanzia majira ya mchana jumla ya nyumba 25 za wakazi wa kitongoji hicho zinadaiwa kubomolewa kwa madai ya kupisha ujenzi wa majosho ya kuogeshea mifugo eneo la kitongoji cha Lukonde chenye ukubwa wa zaidi ya ekari 3,000.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Lukonde, Hamdan Chawila alisema kuwa jumla ya nyumba 25 zimebomolewa na askari polisi ikishirikiana na mgambo ili kupisha ujenzi wa josho la kuogeshea mifugo na kusababisha zaidi ya wananchi 3,00 kukosa sehemu ya kuishi.

Chawila alisema kuwa tukio hilo hakuna kiongozi wa kitongoji hicho ambaye ameshirikishwa jambo ambalo wameshangaa kuona askari pamoja na mgambo wakivamia na kubomoa nyumba hizo huku akieleza kuwa eneo hilo anafahamu kuwa lina mgogoro na anayedaiwa kuwa ni mwekezaji aliyefahamika kwa jina la, Profesa Martin Ndabikunze Shem wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) huku kesi ya msingi ikiwa imefunguliwa katika mahakama ya mwanzo Mikese baada ya mgogoro wa muda mrefu.

“Januari 10 mwaka huu majira ya mchana tulivamiwa na askari polisi wakiwa na mgambo na kubomoa nyumba 25 katika kitongoji changu na kusababisha wananchi zaidi ya 3,00 kukosa sehemu ya kuisha na kufanyika kwa uhalibifu wa mali mbalimbali”. Alisema Chawila.

Mmoja wa wahanga wa tukio hilo, Fikiri Mikidadi Buma alisema kuwa tukio hilo la kubomolewa nyumba yake pamoja na wenzake limemrudisha nyuma kimaendeleo ukizingatia tayari alifanikiwa kujenga nyumba iliyoekzwa na mabati.

Buma alisema hakuna taarifa zozote juu ya baada ya kubomolewa nyumba zao katika zoezi la kuwaondoa kwa nguvu lililofanywa na jeshi la polisi, mgambo pamoja na kundi la vijana wanaodaiwa kushiriki katika tukio hilo.

“Ninachojua mimi eneo hili lina mgogoro na mwekezaji na kesi ya msingi ipo mahakama ya mwanzo Mikese lakini nimeshsngazwa kuona askari polisi na mgambo kuvamia nyumba yangu na kuibomoa zikiwemo na nyumba za wenzangu na kupata hasara ya mali na wengine kuibiwa fedha katika tukio hilo la bomoa bomoa”. Alisema Buma.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema kuwa jeshi la polisi halikuhusika katika ubomoaji wa nyumba hizo na badala yake askari wa jeshi hilo walienda katika eneo hilo baada ya kutokea kwa vurugu baina ya wananchi na wanamgambo aliodai walikuwa wanatekeleza amri ya baraza la nyumba la halmashauri ya wilaya ya Morogoro kubomoa nyumba eneo hilo.
Kwa hisani ya Juma Mtanda Blog
Read More >>

Friday, January 3, 2014

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKIWA MAPUMZIKONI JIMBONI KWAKE

IMG_0647
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua shmaba la mahindi katika  kijiji cha Mamba wilayani Mlele akiwa katika mapumziko, jimboni kwake Katavi Januari 2, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Read More >>

hapa ndio Sehemu atakapozikwa marehemu Dk William Mgimwa kijijini Magunga


Katibu wa mbunge Dr Wiliam Mgimwa Bw Martine Simangwa akiwaonyesha viongozi  wa  CCM eneo ambalo waziri Mgimwa atazikwa  katika  kijiji  cha Magunga kata  ya Maboga  jimbo la Kalenga. 




Read More >>

Mauaji ya Kutisha Ya Mlinzi wa Sengo Morogoro

KUMRADHI KWA MUONEKANA WA PICHA HII.
MWILI wa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Sengo Morogoro, Juma Mazengo ukiwa umefungwa kamba nyuma ya mgongo wake baada ya watu wasiofahamika kumvamia na kumuua katika lindo usiku wa manane wa januari 02/2014 katika ghala la kampuni ya bie ya Serengeti, ghala ambalo lipo nyuma ya gereji ya Abood Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro ambapo eneo la tukio mwili huo ulikuwa umekutwa umefungwa kamba na kutapakaa damu.PHOTO/MTANDA BLOG

Kando ya mwili wa marehemu Mazengo ilikuwatwa bisibisi iliyolowa damu huenda ikawa imetumika katika mauaji hayo ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo, silaha aina ya bunduki bado haijaoenekana na kudhani huenda wahalifu hao wameondoka nayo, jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa tukio hilo ili sheria kuweza kuchukua mkondo wake. PHOTO/MTANDA BLOG
Read More >>

Wednesday, July 31, 2013

ANGALIA PICHA ZA ZIARA YA WAZIRI MKUU WA THAILAND BI YINGLUCK SHINAWATRA KATIKA HIFADHI YA SERENGETI MKOANI MARA


 Mkurugenz wa TANAPA Allan Kijaz akisalimiana na Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra



 Maandalizi ya Mapokezi ya Waziri Mkuu waThailand Yingluck Shinawatra.
Na Mwana wa Afrika Blog

 Makanda wakiwa tayar kwa Mapambano

 Waziri wa Mali asili na Utalii nchini Baloz Hamis Kagasheki akipokewa na Mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijaz

  Waziri wa Mali asili na Utalii nchini Baloz Hamis Kagashek wakikumbatiana kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Tuppa
Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...