Kutoka
kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba
Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya
viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni
ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa
mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF
leo jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa
mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF
leo jijini Dar es Salaam.

Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.

Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto)
akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara
baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa
wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.

Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu
wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango
maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo
jijini Dar es Salaam.

Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu
ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu
ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu
ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.
WAZIRI
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ameipongeza Benki ya Posta Tanzania
(TPB) kwa kuandaa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko
wa Pensheni wa LAPF ikiwa ni fursa itakayowainua kiuchumi wastaafu hao.
Waziri Kabaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa rasmi mpango wa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF, mpango utakaowawezesha wastaafu sasa kuchukua mikopo na kuendelea kukidhi maitaji yao kipindi hicho. Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Waziri Kabaka alisema Benki ya Posta na Mfuko wa Penseni wa LAPF hauna budi kupongezwa kwa hatua ya kulikumbuka kundi la wastaafu ambalo kimikopo lilikuwa limesahaulika.

“…Naomba
nichukue nafasi hii kuwashukuru Benki ya Posta Tanzania pamoja na Mfuko
wa Pensheni wa LAPF kwa kubuni mpango huu maalum wa kuwasaidia wastaafu
kimaisha na kuwawezesha kumudu gharama za mahitaji yao na kukabiliana
na ukosefu wa muda mfupi wa fedha wanazohitaji kwa kuwapatia mikopo,”
alisema Waziri Kabaka.
Aliongeza
kuwa mpango huo utawasaidia wastaafu kipindi cha maisha yao mapya ya
kustaafu kwani licha ya muda huo wengi kuwa na kipato kidogo cha mapato
lakini gharama za maisha kwao hazipungui na badala yake huendelea
kupanda, jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwao.
“…Ninafarijika
kuona kwamba Benki ya Posta pamoja na LAPF mmeliona hili na kulifanyia
kazi, na hatimaye kuja na huduma hii ya mikopo. Lengo mahususi la mpango
huu ambao kwa kiasi fulani umeanza kutekelezwa ni kuwapa faraja na
kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali, ili kuweza
kuboresha maisha yao na maslahi kwa ujumla,” alisema waziri huyo.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla hiyo, alisema mkopo huo ni wa kwanza na wa aina yake katika soko la mabenki nchini hivyo wanaamini utatoa hauweni kwa wastaafu wa LAPF.
Akifafanua zaidi alisema mstaafu anayehitaji kuwa na dhamana huku riba inayotozwa kwa mkopo huo kuwa ni ndogo yaani asilimia 12 tu kwa mwaka ukilinganisha na mikopo mingine. “…Mkopo huu umewekewa bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea kudaiwa. Hivyo wastaafu wote wa mfuko wa LAPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu,” alisema Moshingi.

Alisema
huduma za mikopo hiyo ni za haraka na bora na zitatolewa kwa matawi
yote ya Benki ya Posta Tanzania hivyo kuwataka wahitaji wote wastaafu wa
Mfuko wa Penseni wa LAPF kwenda katika matawi hayo popote nchini kupata
maelezo ya nini cha kufanya kabla ya kupata mkopo huo.
Hata
hivyo TPB kwa kushirikiana na LAPF wamezishauri taasisi za fedha
nyingine zikiwemo Benki kuangalia namna ya kuweka mipango ya kusaidia
wastaafu nchini kwani kundi hilo lina kiasi kikubwa cha fedha ambacho
kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchango mkubwa katika uchumi wan chi ya
Tanzania. Hafla hiyo pia iliyohudhuriwa na viongozi waandamizi na
wafanyakazi wa TPB na Mfumo wa Penseni wa LAPF ilishirikisha pia baadhi
ya wastaafu ambao baadhi walieleza wameanza kunufaika na mpango huo wa
mikopo kwa wastaafu.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
*Imeandaliwa na www.thehabari.com