Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed
akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Vuga kuhusu Ugonjwa wa Ebola na
mikakati ambayo SMZ inaendelea kuichukuwa ili kukabiliana na ugonjwa huo
hatari, hadi sasa hakuna mgonjwa alieyegundulikana na ugonjwa huo
Zanzibar.
Wandishi
wa Habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mohammed Aboud
alipokuwa akitoa tarifa juu ya ugonjwa hatari wa Ebola Ofisini kwake
Vuga Mjini Zanzibar. Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed
akifafanua kitu wakati wa Mkuta wake na wanahari. Picha na Makame
Mshenga- Maelezo Zanzibar.
NA/JAMILA ABDALLA –MAELEZO ZANZIBAR.
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imeanza kuchukua hatua mbali mbali za
kukabiliana na Ugonjwa hatari wa Ebola ambao unazidi kusambaa katika
nchi mbali mbali Barani Afrika.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohamed
ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ofisini kwake Vuga
mjini Zanzibar kuhusiana na mikakati ambayo SMZ inaichukua ili
kukabiliana na ugonjwa huo.
Waziri
Aboud amesema licha ya kwamba Zanzibar hakuna Mgonjwa aliyegundulika
kuwa na Ebola lakini mazingira yanaonesha kuwa Zanzibar inaweza kupata
maradhi hayo kutokana na kuwa na muingiliano mkubwa na nchi nyingine
ambazo tayari zimethiriwa na Ugonjwa huo.
Ametaja
mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo
vya habari juu ya maradhi ya Ebola na namna ya kujikinga.
Mh:
Aboud amesema kuwa pia serikali itaimarisha taratibu za ugunduzi
,ukaguzina ufuatiliaji wa washukiwa wa ugonjwa huu katika bandari
,viwanja vya ndege,vituo vya afya na jamii kiujumla.
Akiendelea
kufahamisha mikakati hiyo waziri huyo amesema kuwa Pia serikali
imeandaa maeneo maalumu kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa Ebola ambapo
wizara ya Afya watayatangaza hivi karibuni.
Pamoja
na mikakati hiyo waziri Aboud amewaomba waandishi wa habari kusaidia
katika kusambaza elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huo.
Akitaja
dalili za ugonjwa huo Waziri Aboud amesema kuwa dalili kuu ni homa,
maumivu makali ya kichwa, misuli na viungo vya mikono na miguu pamoja na
koo.
Dalili
nyengine ni kukosa nguvu za kiwiliwili na kufuatiwa na vipele katika
ngozi,macho kuwa mekundu na kutokwa na damu katika tundu mbalimbali za
mwili ikiwemo pua ,masikio mdomo na ngozi.
Kwa
upande mwengine waziri ametaja njia zinazotumika kusambaza ugonjwa huo
kuwa ni kugusana mojakwa moja na mtu aliyeambukizwa ,kugusa majimaji
yanayotokana na mgonjwa kama vile damu,jasho, mate ,mkojo na
makohozipamoja na kutumia vifaa vilivyotumiwa na mgonjwa mwenye
maambukizi bila kusafisha vizuri.