Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, August 18, 2014

SERIKALI YAJIZAJITITI KUSIMAMIA HAKI ZA MTOTO NA MAREKEBISHO YA TABIA.

 SAM_0080Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Steven Gumbo (kushoto) akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia haki za mtoto na marekebisho ya tabia leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. 
SAM_0131Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Nsachris Mwamwaja (kulia) akikanusha taarifa zilizo ripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuhusu uwepo wa wagonjwa wa Ebola pamoja na hatua za tahadhari zilizochukuliwa na serikali ikiwemo kupeleka vifaa tiba kote nchini.Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Daniel Masunzu
SAM_0073
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Frank Mvungi)
Na Frank Mvungi
Serikali imejizatiti katika kutekeleza mpango wa majaribio wa marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria katika jamii.
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bw. Steven Gumbo wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
 
 “Serikali imefanikiwa kukamilisha kanuni za mahabusu za watoto, makao ya watoto na shule ya maadilisho” alisema Gumbo.
 
Pia hatua nyingine ni kukamilika kwa miongozo ya utoaji wa huduma katika mahabusu za watoto na shule ya maadilisho.
 
Hatua nyingine ni kuwepo kwa mwongozo wa  kijamiii (CRP)  wa Marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na walio katika hatari ya kukinzana na sheria.
 
Mafanikio mengine ni kuwajengea uwezo watumishi wote wa mahabusi za watoto na shule ya maadilisho juu miongozo mbalimbali iliyotolewa ya kuboresha huduma katika Taasisi hizo.
Akieleza zaidi Gumbo amesema kwa mujibu wa sheria ya mtoto, wanaokinzana na sheria na ambao hawajapata dhamana kutoka katika mahakama wanapaswa kupelekwa katika mahabusi za watoto, pale ambapo mahakama imejiridhisha kuwa mtoto huyo ametenda kosa huamuru apelekwe katika shule ya maadilisho.
Wizara ya Afya kupitia idara ya Ustawi wa jamii imekuwa ikishirikiana na wadau mblimbali kama vile Polisi, Mahakama, Magereza, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake.
 
Watoto wanaokinzana na sheria wanatunzwa katika mahabusi tano za watoto zilizopo katika mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya na Dar es salaam na katika shule ya maadilisho ya Irambo-Mbeya.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...