Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Showing posts with label tanzia. Show all posts
Showing posts with label tanzia. Show all posts

Wednesday, January 15, 2014

WAENDESHA BODABODA UYOLE WAKIMBIA NA MAITI YA MWENZAO BAADA YA MCHUNGAJI KUWAAMBIA WAMEFWATA UBWABWA



 Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.


 Kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole

Marehemu Gabriel Osward Ngalele. enzi za uhai wake


Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani


Katikati mke wa Marehemu

Mwili wa marehemu ukiagwa makaburini hapo


Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.





Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.

Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa na Roli.

Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika Ibada.

Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea mtafaruku mkubwa.

Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.

Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi.

Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara kwa mara.

Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na si waumini wa Kanisa lake.

Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.

Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.

Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.

Na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
Read More >>

Sunday, December 1, 2013

TAARIFA NA VIDE0 YA AJALI YA KIFO CHA MUIGIZAJI POUL WALKER

  Paul-Walker-Wallpaper-paul-walker-25716655-1024-768

Wapenzi wa movie za The Fast and the Furious watakuwa wanamfahamu Paul Walker vizuri ambapo ameshiriki kikamilifu kwenye movie za Fast and Furious.
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao hadi ku-trend kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ni kuhusu kifo cha muigizaji huyu ambapo taarifa rasmi zinasema alikuwa anatoka kwenye event ya kujitolea ya organisation yake inaitwa Reach out World Wide.
Paul Walker akiwa kwenye safari ya kurudi kutoka kwenye hiyo event ndani gari la kifahari lenye viti viwili aina ya Porsche Carrera GT, ambapo yeye alikuwa abiria na rafiki yake akiwa dereva wa gari hilo ndio wakapata  ajali.
Habari zinasema kwamba dereva huyo alipoteza control na kuvamia mti au nguzo na gari kuanza kuwaka moto.
Polisi hawajathibisha rasmi chanzo cha ajali hiyo lakini hadi hivi sasa inasemekana kuwa ni speed kali ambayo ilimfanya dereva ashindwe ku-control gari hilo.
Paul amefariki akiwa na miaka 40 na ameacha binti mwenye miaka 15
Wadadisi wa mambo ya kibiashara wameshaiangalia Fast and Furious 7 kwamba itafanya vizuri sokoni kwasababu hiyo ndio itakuwa movie ya mwisho ya Paul Walker na itatoka July 11, 2014.hg 
Hii picha ilipigwa muda mfupi kabla ya ajali kutokea akiwa anaondoka kwenye event ya kujitolea na hilo ndio gari lenyewe kabla ya ajali
1130-paul-walker-accident-scene-car-facebook-3 
Gari baada ya ajali na moto kuzimwa
1130-paul-walker-fan-twitter-picture-article-7
Picha hii alipiga na kwenye tukio hilo
fast-furious-6 
Juu na chini ni baadhi ya scenes Paul Walker alizoshiriki kwenye Fast and Furious
Read More >>

Wednesday, July 31, 2013

Ibra wa “Wakali Danta” auawa kwa kuchomwa kisu ktk kugombania demu aitwaye Fatma Kiduku

WAKATI Waislamu wakiwa ndani ya Mfungo wa Ramadhani, mapenzi yamemuua kijana Ibrahim Ibrahim ‘Ibra’ wa Kundi la Wakali Danta la Magomeni jijini Dar kwa kuchomwa visu.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 27, mwaka huu maeneo ya Magomeni Kagera ambapo ndugu wa Ibra, Ally Jumanne Sanane alidai kuwa, Ibra alichomwa kisu na kijana aliyefahamika kwa jina la Kelvin wakimgombea demu aitwaye Fatma Kiduku.
Mtoa habari huyo alidai: “Fatuma alikuwa ni mchumba wa Ibra lakini pia inaonekana alikuwa akitoka na Kelvin.
Sehemu ya waombolezaji.
“Siku ya tukio Kelvin alikutana na Fatuma, akamuanzishia vurugu akimuuliza sababu ya kumuacha yeye ili aolewa na Ibra. Vurugu ilikuwa kubwa, Fatuma akaamua kumuita Ibra ili amsaidie.
“Ibra alipofika ndiyo akaanza kupigana na Kelvin, kuona amezidiwa Kelvin alitoa kisu na kumchoma cha kwanza kisha cha pili na ndiyo Ibra akaanguka chini na hakuamka tena,” alidai mtoa habari huyo.
Marehemu Ibra enzi za uhai wake.
Baada ya tukio hilo inadaiwa Kelvin na Fatuma walikimbia hadi tunakwenda mitamboni hawakuwa wamepatikana.

 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 27, saa 9:30 eneo la Brazil Magomeni Kagera.
Kamanda Wambura alisema kuwa Kelvin ambaye anahusika na mauaji hayo anasakwa na jeshi la polisi.
Mbali na Kelvin pia  mwanamke ambaye ndiye chanzo cha tukio hilo naye anasakwa.
Kesi hiyo imefunguliwa jalada namba MAG/IR/5600/ 2013 MAUAJI.
Uchunguzi wa jeshi la polisi unaendelea zaidi ili kuweza kuwakamata wahusika waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Waombolezaji wakiwa na simanzi.
SOURCE-GPL
Read More >>

Saturday, July 20, 2013

BREAKING NEWZZZ:MR BOMBA ALIYEKUA ANAIGIZA KAOLE GROUP AMEFARIKI DUNIA



Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba msanii wa muda mrefu wa kundi la kaole unayemuona katika picha maarufu kwa
jina la Mr Bomba amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa tatizo la muda mrefu la kansa ya uvimbe katika ini.Mungu alitoa Mungu ametwaa Jina la bwana lihimidiwe.Amina

Endelea kutembelea mtandao huu tutakujuza zaidi kitakachojili
Read More >>

Tuesday, July 16, 2013

DK SHEIN AMPA POLE MWAMUNYANGE

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
     Zanzibar                                                                                              16.7.2013
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,  pamoja na wananchi wa Zanzibar wamepata mshtuko na huzuni kubwa kwa vifo vya wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi wa Watanzania walioshambuliwa na kuuawa wakati walipokuwa wakilinda amani katika eneo la Darfur, nchini Sudan.
Dk. Shein ameelezea kusikitishwa kwake na vifo hivyo na kueleza kuwa inasikitisha zaidi kuwa wanajeshi hao wamekufa wakiwa katika kazi ya kulinda amani nchini humo na kueleza kuwa wao ni mashujaa na wamekufa kishujaa.
Hayo yalielezwa katika salamu zake za  rambi rambi alizotuma Dk. Shein kwa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananachi wa Tanzania, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange pamoja na wanajeshi wote, pia, salamu hizo zilitoa pole kwa familia za wafiwa.

Aidha, salamu hizo alizozituma Dk. Shein zilieleza kuwa huu ni msiba wa Taifa lote na wananchi wote wa Zanzibar wanaungana pamoja katika kuomboleza msiba huo.

“Tunatoa pole na tunamuomba MwenyeziMungu aziweke pahala pema peponi roho za mashujaa hao, vile vile tunawatakia nafuu ya haraka majeruhi wote wa tukio hilo”.

Alisisitiza Dk. Shein “ Mwenyezi Mungu akupeni moyo wa subira na ustahamilivu katika kipindi hiki cha msiba mkubwa”. zilieleza salamu hizo za rambirambi

Dk. Shein pamoja na wananchi wa Zanzibar wanaungana na Watanzania wenzao kuwaombea wale wote walioumia katika tukio hilo ili waweze kupona kwa haraka na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani.

 Vijana saba wa Jeshi la Wananachi wa Tanzania waliuawa baada ya kushambuliwa na waasi wa Sudan na wengine walijeruhiwa.

Wanajeshi hao wa Tanzania waliopoteza maisha yao pamoja na wale walioumia walikuwa ni sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika eneo la Darfur.

Katika suala la ulinzi wa amani katika eneo hilo la Darfur, Wanajeshi kutoka Tanzania wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya ulinzi tokea pale Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mnamo mwaka 2007, ambapo vijana hao waliouawa ni miongoni mwa vijana waliokwenda nchini humo Februari mwaka huu.

 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Read More >>

Monday, July 15, 2013

PRAN KRISHAN GWIJI LA FILAMU INDIA AFARIKI AKIWA NA MIAKA 93

VETERANI wa filamu Nchini India, Pran Krishan Sikand, maarufu kama Pran, amefariki dunia katika hospitali ya Lilavati jijini Mumbai Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 93 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pran ambaye amedumu katika sanaa hii ya uigizaji kwa zaidi ya miaka 60, alikuwa maarufu kwa kucheza sehemu ya mtu katili – adui katika filamu za Kihindi.
Kati ya miaka ya 1960 na 1980, alionekana karibu katika kila filamu kali ya Bollywood, na alishinda tuzo nyingi katika kazi yake ikiwamo kubwa na maarufu ya Dadasaheb Phalke Award.
Pran amecheza filamu zaidi ya 350, maarufu zaidi ikiwa Zanjeer iliyotoka mwaka 1973 ambayo alipambana na mkongwe mwingine wa Bollywood, Amitabh Bachchan.

Read More >>

Saturday, July 13, 2013

MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI DUNIA AKIWA ANAOGELEA KATIKA BAHARI YA HINDI...!

Picture
Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi wa Kompyuta wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Wendy Habakuki Lwendo amefariki dunia katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni akiogelea na wenzake watatu jana jioni.

Taarifa kutoka kwa  kaka wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao alipatwa na masaibu hayo akiwa na rafiki zake hao watatu wakiogelea baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika eneo la kina kifupi cha maji yaliyokupwa na mara maji hayo yaka jaa na walipokuwa wakijaribu kutoka ndipo Wendy akazidiwa na maji.

Lwendo amesema kuwa wenzake walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake tayari ilikuwa mbaya na kwakuwa hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu 

aliyezama majini walihangaika kwa zaidi ya dakika 40 kumsaidia ndipo wakapata msaada wa Polisi  kumkimbiza kituo cha afya Kibaoni huko Kigamboni lakini jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.

Aidha alisema kuwa mwili wa Marehemu ulihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya Vijibweni na sasa ndugu wamefika na kuhamishia mwili huo Hospitali ya jeshi Lugalo.

Msiba kwa sasa upo Kinondoni nyuma ya Vijana, huku wakisubiriwa wazazi wa marehemu pamoja na ndugu wengine ili kujua taratibu kamili za maziko.

Wazazi wa Wendy, Mchungaji Habakuki Lwendo ni mwalimu wa Chuo cha Uchungaji Makumira mkoani Arusha.

Source: Father Kidevu blog
Read More >>

Thursday, July 11, 2013

ALIYEFARIKI SIKU YA HARUSI YAKE AZIKWA NA MWANAE.

ROMBO, Ilikuwa ni majonzi, vilio na huzuni katika kijiji cha Mahalu, wilayani Rombo, Kilimanjaro kufuatia mazishi ya aliyetarajiwa kufunga ndoa Jumamosi marehemu Levina Swai pamoja na mwanawe.
Marehemu Levina alizikwa na mwanaye kaburi moja baada ya kichanga hicho kufariki siku hiyo hiyo mara baada ya mama yake kupoteza maisha kwa kile kilichodaiwa ni kuugua Malaria, shinikizo la damu kuwa chini na upungufu wa damu.
Marehemu Levina alifariki wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Akizungumza katika kijiji cha Mahalu kata ya Makiidiwilayani Rombo, alikozikwa,wifi wa marehemu, Hortensia Mrima alisema wifi yake alifia hospitalini na alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Nndawa mkoani Lindi akiwa katika mpango wa ajira ya walimu wapya.
“Mimi ndiye nilikuwa namuuguuza hospitalini tangu Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbuliwa na malaria na kupungukiwa na damu na pressure (shinikizo la damu) kuwa chini,”alisema Mrima.
Ibada ya mazishi ilianza saa 8:30 mchana ikiongozwa na Padri Emmanuel Mavengero na kuhudhuriwa na waombolezaji kutoka Tanga na Kilimanjaro.
Mazishi hayo yalitawaliwa na simanzi huku waombolezaji wengi akiwamo aliyetarajiwa kumuoa marehemu Levina,Gabriel Swai muda wote alikuwa akibubujikwa na machozi na kushindwa kuzungumza.
Wifi huyo alieleza kuwa wifi yake alipopimwa alikutwa na Malaria 13 na kupewa dawa za malaria za SP na dripu za Quinine ambazo zilimlewesha sana na kuendelea kudhoofu.
“Siku hiyo ya Alhamisi alikata kauli akawa haongei ikabidi daktari amwekee dripu za Glucose ili kumuongezea nguvu na shinikizo la damu ilirudi sawasawa lakini bado alikuwa amelegea na alikuwa haongei,”alisema.
Ilipofika Jumamosi ambayo ndiyo siku iliyokuwa imepangwa kufunga ndoa na Gabriel Swai, ikabidi madaktari wamuwekee maji ya uchungu ili kumuokoa mtoto baada ya mama kuwa mahututi.
“Yale maji ya uchungu yalimsaidia akaweza kujifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 1.7 na baada ya kujifungua alipoteza fahamu na saa 8:05 mchana akafariki dunia,”alisema.
Kwa mujibu wa Mrima, mtoto aliendelea kuishi huku akipewa maziwa lakini alikuwa akiyatapika, hadi ilipofika saa 5:00 usiku alifariki dunia.
Read More >>

TANZIA: Mama mzazi wa PROF JAY amefariki dunia usiku..!


Hali ilivyo asubuhi hii hapa nyumbani kwa Prof Jay ambapo ndipo ulipo msiba wa mama yetu.. kwa wanaotaka kuja msiba upo Mbezi mwisho baada ya stendi mpya ya mabasi basi mbele kidogo mkono wako wa kushoto utaingia utaona nyumba kumba ipo kwa chini na magari mengi basi ndio hapo hapo. Kwa wanaokuja na daladala baada yakupita hiyo stendi mpya utamwambia konda akushushe kwa Prof Jay maana ndio kituo hicho. RIP MAMA MAJANJALA
Read More >>

Wednesday, July 10, 2013

Msanii Z anto afiwa na mama yake mzazi

Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa msanii Z Anto amefiwa na mama yake mzazi masaa machache yaliyopita, akiwa katika hospitali ya muhimbili ambapo alikuwa amempeleka masaa mawili yaliyopita.
Nw nipo muhimbili nmemleta mama hali yake c nzuri kabisa, ingawa kuumwa sio kufa ila kwa hali aliyonayo lolote laweza kutokea. naomben dua zenu ndugu zangu.
akiongea na blog hii dakika chache zilizopita Z Anto amesema Mama yake, alikuwa anasumbuliwa na cancer ya ini kwa muda mrefu, lakini kwa takribani miezi miwili iliyopita hali yake ilianza kubadilika, na leo hii walimpeleka hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambapo alifariki muda mchache baadae.
Pole sana kwa Z Anto, familia nzima, ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu uliowafika.
Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi ameen.
Read More >>

Saturday, July 6, 2013

WAZIRI MKUU PINDA AONGOZA MAZISHI YA DIWANI CHONANGA IRINGA, AJITOLEA KUSOMESHA FAMILIA YAKE HUKu AKISIFU USHIRIKI WA CHADEMA KATIKA MAZISHI

Mmoja kati ya madiwani wa Manispaa ya Iringa akiwa ameshika picha ya marehemu diwani Chonanga
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (mwenye Suti) na katibu wa Chadema Iringa mjini Suzana Mgonakulima wa kwanza kushoto wakiwa na madiwani wa CCM katika msiba wa diwani Chonanga leo
Msaidizi wa askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Gavile akiendesha ibada ya mazishi ya diwani Chonanga leo makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Hili ni gari ambalo lilkuwa likiufuata msafara wa waziri mkuu jambo ambalo lingeweza kusababisha ajali katika msafara huo hapa ni eneo la Mtwivila mjini Iringa
Msafara wa waziri mkuu Mizengo Pinda ukielekea makaburi ya Mtwivila kuongoza mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Iddi Rashid Chonanga leo
Mwili wa marehemu Chonanga ukishusha kaburini na madiwani wa Manispaa ya Iringa
 



Mlezi wa CCM mkoa wa Iringa waziri mkuu Mizengo Pinda (kushoto ) mkewe Tunu Pinda wakiweka shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga leo
Waziri mkuu Pinda akimsubiri mke wake Tunu Pinda aweke shada ya maua kabla ya kutoa heshima yao ya mwisho leo

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akiweka shada la maua katika kaburi ya diwani Chonanga leo
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wakishirikiana kuweka shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga ,enzi za uhai wake diwani Chonanga na familia yake walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kumtishia kumuua mbunge Msigwa kwa maneno kesi ambayo bado hukumu yake kutolewa
Mbunge wa jimbo la Kilolo na MNEC Prof Peter Msolla na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu wakiweka shada la maua katika kaburi la Chonanga leo

Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akipokea shada kutoka kwa afisa habari Manispaa ya Iringa Sima Bingileki ili kuweka katika kaburi la diwani Chonanga
Meya Mwamwindi akiweka shada la maua katika kaburi la Chonanga
Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Bw Gervas Ndaki kushoto akiongoza madiwani kuweka mashada ya maua katika kaburi la diwani Chonanga leo
Katibu wa Chadema Iringa mjini na diwani wa viti maalum Suzana Mgonakulima kushoto akiweka shada la maua katika kaburi la Diwani mwenzake Chonanga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo akiweka shada la maua leo kwenye kaburi la diwani Iddi Chonanga

Picha na habari na Francis Godwin Blog- Mzee wa matukio Daima


WAZIRI mkuu Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa leo ameongoza wakazi wa mkoa wa Iringa katika mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Iddi Rashid Chonanga huku akijitolewa kusomesha watoto wake wawili na yatima mmoja aliyekuwa akisomeshwa na marehemu Chonanga.


Waziri Pinda alitoa ahadi leo katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa wakati akitoa salam zake za rambi rambi kwa wakazi wa kata ya Nduli na wananchi wa mkoa wa Iringa kufuatia kifo cha diwani huyo .


Alisema kuwa kifo cha diwani Chonanga kimeacha pendo ndani ya familia na hata katika chama chake cha CCM kutokana na mchango mkubwa ambao amepata kuutoa katika kupigania chama hicho na kuwa kutokana na maombi kusomeshwa yaliyotolewa na watoto hao ambao waliyatoa jana alipofika kuhani msiba huo katika kijiji cha Nduli


Kuwa kwa upande wake amejitolea kuisaidia familia hiyo ya Chonanga kwa kusomesha mtoto mmoja anayeendelea na masomo katika chuo cha IFM jijini Dar es Salaam pia kumsomesha kijana wake mmoja ambae yupo sekondari pamoja na kuendelea kumsomesha mtoto mmoja yatima ambae diwani Chonanga alikuwa akimsomesha katika shule ya Sekondari ya Miyomboni mjini Iringa.


Mbali ya kujitolea kusomesha watoto hao bado waziri Pinda alilitaka baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kumuenzi diwani Chonanga kwa kazi kubwa za maendeleo alizozifanya katika kata yake kwa kuisaidia familia yake .


“ Mimi nawashauri madiwani pamoja na mkurugenzi wa Manispaa kutokana na mchango mkubwa ambao diwani Chonanga aliutoa katika kuwatumikia wananchi wa kata ya Nduli ….sasa kuangalia uwezekano wa kuisaidia familia yake…..sisi kama chama leo tulikuwa na Halmashauri kuu ya CCM tumechangishana kiasi cha zaidi ya Tsh 800,000 ambazo tunazikabidhi kwa familia”


Katika hatua nyingine waziri Pinda amekipongeza chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini chini ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika mazishi hayo .


“ Kweli kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwashukuru sana viongozi wa Chadema Iringa chini ya mbunge mchungaji Msigwa kwa ushiriki mzuri wa mazishi ya diwani Chonanga ….nasema ahsanteni sana mheshimu mbunge Msigwa na wananchi wote ambao leo mmefika hapa”



Awali akiendesha ibada ya mazishi hayo msaidizi wa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Tuluwene Gavile alitaka viongozi wa serikali na kisiasa kukumbuka kumcha Mungu na kuiga mfano wa Chonanga ambae mbali ya kufanya shughuli za kisiasa ila katika dini alikuwa mstari wa mbele akiwa kama mshauri wa usharika wa Nduli .



Alisema kuwa mara kwa mara Chonanga alikuwa akipigania maendeleo ya kata yake ya Nduli na wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania wananchi wake.


“ Marehemu alikuwa mtetezi wa kweli wa maendeleo ya wananchi wake ndani ya chama chake na hata katika kanisa pia ndio maana leo umati mkubwa wa watu wamejitokeza kumzika ila sisi kama kanisa tunasema kifo katika Kristo ni furaha kubwa na leo hii mama mzazi wa Chonanga ambae ana miaka zaidi ya 83 ameomba kubatizwa rasmi “



Akisoma histori ya marehemu Chonanga mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo alisema kuwa Chonanga alizaliwa mwezi Februari ,1947 katika kijiji cha Malolo wilaya ya Kilosa na elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya kati ( Middle School ) Kidodi wilaya ya Kilolo na kujiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Songea mkoani Ruvuma mwaka 1970



Katika uhai wake marehemu aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi mwaka 1972 ambapo miongoni mwa shule alizopata kufundisha ni pamoja na Mwembetogwa ,Kilimani , Nyabula, Nduli na Kitelewasi zilizopo mkoani Iringa pia marehemu aliwahi kuwa mratibu elimu kata ya kalenga kuanzia mwaka 1994-1999 alipostaafu kwa mujibu wa sheria na mwaka 2000 alifanya kazi ya ualimu kwa mkataba wa mwaka mmoja


Katika uongozi amepata kuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Nduli kati ya mwaka 2000-2005 na mwaka 2010 alichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Nduli katika Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Iringa na katika baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi .


Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake alikuwa ni jasiri ,mfuatiliaji wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai .



Marehemu Chonanga alianza kusumbuliwa na maradhi ya moyo usiku wa tarehe 2/7/2013 na alfajiri ya tarehe 3/7/2013 alipelekwa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kupata matibabu na mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari ila zilishindikana na majira ya saa 7;45 mchana alifariki dunia .marehemu Chonanga ameacha mjane mmoja watoto 10 na wajukuu 9

Mungu ailaze roho ya marehemu Iddi Rashid Chonanga mahali pema peponi

AMINA
 
 
Imechotwa: Matukio michuzi
Read More >>
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...