Mmoja kati ya
madiwani wa Manispaa ya Iringa akiwa ameshika picha ya marehemu diwani
Chonanga
Mbunge wa jimbo la
Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (mwenye Suti) na katibu wa Chadema Iringa
mjini Suzana Mgonakulima wa kwanza kushoto wakiwa na madiwani wa CCM katika
msiba wa diwani Chonanga leo
Msaidizi wa askofu
wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa
Blaston Gavile akiendesha ibada ya mazishi ya diwani Chonanga leo makaburi
ya Mtwivila mjini Iringa
Hili ni gari ambalo
lilkuwa likiufuata msafara wa waziri mkuu jambo ambalo lingeweza
kusababisha ajali katika msafara huo hapa ni eneo la Mtwivila mjini Iringa
Msafara wa waziri
mkuu Mizengo Pinda ukielekea makaburi ya Mtwivila kuongoza mazishi ya
aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Iddi Rashid Chonanga leo
Mwili wa marehemu
Chonanga ukishusha kaburini na madiwani wa Manispaa ya Iringa
Mlezi wa CCM mkoa
wa Iringa waziri mkuu Mizengo Pinda (kushoto ) mkewe Tunu Pinda wakiweka shada
la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga leo
Waziri mkuu Pinda
akimsubiri mke wake Tunu Pinda aweke shada ya maua kabla ya kutoa heshima
yao ya mwisho leo
Mkuu wa mkoa wa
Iringa Dr Christine Ishengoma akiweka shada la maua katika kaburi ya diwani
Chonanga leo
Mbunge wa jimbo la
Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) na mbunge wa viti maalum mkoa wa
Iringa Ritta Kabati (CCM) wakishirikiana kuweka shada la maua katika kaburi la
diwani Iddi Chonanga ,enzi za uhai wake diwani Chonanga na familia yake
walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kumtishia kumuua mbunge Msigwa kwa maneno kesi
ambayo bado hukumu yake kutolewa
Mbunge wa jimbo la
Kilolo na MNEC Prof Peter Msolla na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa
Lediana Mafulu wakiweka shada la maua katika kaburi la Chonanga leo
Mstahiki meya wa
Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akipokea shada kutoka kwa afisa habari
Manispaa ya Iringa Sima Bingileki ili kuweka katika kaburi la diwani Chonanga
Meya Mwamwindi
akiweka shada la maua katika kaburi la Chonanga
Naibu meya wa
Manispaa ya Iringa Bw Gervas Ndaki kushoto akiongoza madiwani kuweka mashada
ya maua katika kaburi la diwani Chonanga leo
Katibu wa Chadema
Iringa mjini na diwani wa viti maalum Suzana Mgonakulima kushoto akiweka shada
la maua katika kaburi la Diwani mwenzake Chonanga
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo akiweka shada la maua leo
kwenye kaburi la diwani Iddi Chonanga
Picha na habari na
Francis Godwin Blog- Mzee wa matukio Daima
WAZIRI mkuu
Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa
leo ameongoza wakazi wa mkoa wa Iringa katika mazishi ya aliyekuwa diwani
wa kata ya Nduli marehemu Iddi Rashid Chonanga huku akijitolewa kusomesha
watoto wake wawili na yatima mmoja aliyekuwa akisomeshwa na marehemu
Chonanga.
Waziri Pinda alitoa
ahadi leo katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa wakati akitoa salam
zake za rambi rambi kwa wakazi wa kata ya Nduli na wananchi wa mkoa wa
Iringa kufuatia kifo cha diwani huyo .
Alisema kuwa kifo
cha diwani Chonanga kimeacha pendo ndani ya familia na hata katika chama
chake cha CCM kutokana na mchango mkubwa ambao amepata kuutoa katika
kupigania chama hicho na kuwa kutokana na maombi kusomeshwa yaliyotolewa na
watoto hao ambao waliyatoa jana alipofika kuhani msiba huo katika kijiji
cha Nduli
Kuwa kwa upande wake
amejitolea kuisaidia familia hiyo ya Chonanga kwa kusomesha mtoto mmoja
anayeendelea na masomo katika chuo cha IFM jijini Dar es Salaam pia
kumsomesha kijana wake mmoja ambae yupo sekondari pamoja na kuendelea
kumsomesha mtoto mmoja yatima ambae diwani Chonanga alikuwa akimsomesha
katika shule ya Sekondari ya Miyomboni mjini Iringa.
Mbali ya kujitolea
kusomesha watoto hao bado waziri Pinda alilitaka baraza la madiwani la
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuangalia
uwezekano wa kumuenzi diwani Chonanga kwa kazi kubwa za maendeleo
alizozifanya katika kata yake kwa kuisaidia familia yake
.
“ Mimi nawashauri
madiwani pamoja na mkurugenzi wa Manispaa kutokana na mchango mkubwa ambao
diwani Chonanga aliutoa katika kuwatumikia wananchi wa kata ya Nduli ….sasa
kuangalia uwezekano wa kuisaidia familia yake…..sisi kama chama leo
tulikuwa na Halmashauri kuu ya CCM tumechangishana kiasi cha zaidi ya Tsh
800,000 ambazo tunazikabidhi kwa familia”
Katika hatua
nyingine waziri Pinda amekipongeza chama cha Demokrasia na maendeleo
(Chadema) wilaya ya Iringa mjini chini ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika mazishi hayo
.
“ Kweli kwa moyo
mkunjufu kabisa napenda kuwashukuru sana viongozi wa Chadema Iringa chini
ya mbunge mchungaji Msigwa kwa ushiriki mzuri wa mazishi ya diwani Chonanga
….nasema ahsanteni sana mheshimu mbunge Msigwa na wananchi wote ambao leo
mmefika hapa”
Awali akiendesha
ibada ya mazishi hayo msaidizi wa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Tuluwene Gavile
alitaka viongozi wa serikali na kisiasa kukumbuka kumcha Mungu na
kuiga mfano wa Chonanga ambae mbali ya kufanya shughuli za kisiasa ila
katika dini alikuwa mstari wa mbele akiwa kama mshauri wa usharika wa Nduli
.
Alisema kuwa mara
kwa mara Chonanga alikuwa akipigania maendeleo ya kata yake ya Nduli na
wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari
kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania wananchi
wake.
“ Marehemu alikuwa
mtetezi wa kweli wa maendeleo ya wananchi wake ndani ya chama chake na
hata katika kanisa pia ndio maana leo umati mkubwa wa watu wamejitokeza
kumzika ila sisi kama kanisa tunasema kifo katika Kristo ni furaha kubwa na
leo hii mama mzazi wa Chonanga ambae ana miaka zaidi ya 83 ameomba
kubatizwa rasmi “
Akisoma histori ya
marehemu Chonanga mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia
Mahongo alisema kuwa Chonanga alizaliwa mwezi Februari ,1947 katika
kijiji cha Malolo wilaya ya Kilosa na elimu yake ya msingi aliipata katika
shule ya kati ( Middle School ) Kidodi wilaya ya Kilolo na kujiunga na
mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Songea mkoani Ruvuma mwaka
1970
Katika uhai wake
marehemu aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi mwaka 1972 ambapo
miongoni mwa shule alizopata kufundisha ni pamoja na Mwembetogwa ,Kilimani ,
Nyabula, Nduli na Kitelewasi zilizopo mkoani Iringa pia marehemu aliwahi
kuwa mratibu elimu kata ya kalenga kuanzia mwaka 1994-1999 alipostaafu kwa
mujibu wa sheria na mwaka 2000 alifanya kazi ya ualimu kwa mkataba wa mwaka
mmoja
Katika uongozi
amepata kuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Nduli kati ya mwaka 2000-2005 na
mwaka 2010 alichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Nduli katika Halmashauri hiyo
ya Manispaa ya Iringa na katika baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo alikuwa
ni mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi
.
Mkurugenzi huyo
alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake alikuwa ni jasiri ,mfuatiliaji
wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai
.
Marehemu Chonanga
alianza kusumbuliwa na maradhi ya moyo usiku wa tarehe 2/7/2013 na alfajiri
ya tarehe 3/7/2013 alipelekwa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kupata
matibabu na mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari ila zilishindikana
na majira ya saa 7;45 mchana alifariki dunia .marehemu Chonanga ameacha mjane
mmoja watoto 10 na wajukuu 9
Mungu ailaze roho
ya marehemu Iddi Rashid Chonanga mahali pema peponi
AMINA
Imechotwa: Matukio michuzi