VETERANI
wa filamu Nchini India, Pran Krishan Sikand, maarufu kama Pran,
amefariki dunia katika hospitali ya Lilavati jijini Mumbai Ijumaa
iliyopita akiwa na umri wa miaka 93 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pran
ambaye amedumu katika sanaa hii ya uigizaji kwa zaidi ya miaka 60,
alikuwa maarufu kwa kucheza sehemu ya mtu katili – adui katika filamu za
Kihindi.
Kati ya
miaka ya 1960 na 1980, alionekana karibu katika kila filamu kali ya
Bollywood, na alishinda tuzo nyingi katika kazi yake ikiwamo kubwa na
maarufu ya Dadasaheb Phalke Award.
Pran
amecheza filamu zaidi ya 350, maarufu zaidi ikiwa Zanjeer iliyotoka
mwaka 1973 ambayo alipambana na mkongwe mwingine wa Bollywood, Amitabh
Bachchan.