KUSHOTO: John Eccles baada ya kuondolewa sehemu ya fuvu lake. KATIKATI: Eccles akiwa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa fuvu lake. KULIA: Andrew Dodds. |
Mtu mmoja
alilazimika kuondolewa theluthi moja ya fuvu lake baada ya kuwa
ameshambuliwa na rafiki yake wa zamani aliyegeuka mshindani wake katika
mapenzi.
Wafanyakazi
wa matibabu walilazimika kupachika kipande cha bati katika kichwa cha
John Eccles baada ya kupondwa fuvu lake ukutano katika makabiliano hayo
yaliyomwacha akiwa hajitambui kwa wiki mbili.
Mtu huyo
mwenye miaka 35 alisema aliachwa kama alikuwa 'kagongwa na gari' wakati
mwishowe alipozinduka hospitali hapo, ambako alilazimishwa kukaa kwa
miezi sita.