Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bw, David Misime ……………………………………………………………………….. Na. Luppy Kunga’lo Polisi Dodoma
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili wenye asilia ya
kiarabu na watanzania watatu kwa tuhuma za kufanya utapeli na kujipatia
fedha kwa njia ya udanganyifu katika vituo vya kuuzia mafuta (sheli) na
maduka ya kubadilishia fedha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bw, David Misime alisema Tukio hilo
lilitokea juzi katika Sheli ya Camel Iliyopo karibu na Chuo Cha Mipango
katika manispaa ya Dodoma.
Kamanda
Misime alisema watu hao walifika katika sheli hiyo ambapo kulikuwa na
duka na kuagiza soda kisha baadae kutoa dola ya kimarekani ya USD 50,
ambapo muuzaji aliwaambia kuwa habadilishi pesa, hivyo kuamua
kumdanganya kuwa wanahitaji pesa ya kitanzania kwa ajili ya kwenda
kuonyesha Misri kama sehemu ya maonyesho.
“Wateja
hao waliomba wapatiwe noti za 10,000/= za zamani ili wao wampatie noti
mpya za 10,000/=, muuzaji huyo alichambua noti za zamani zipatazo
shilingi 470,000/= na kuwapa kisha wao kumwambia wanazotaka
kumbadilishia ziko kwenye gari na kujifanya kwenda katika gari na
matokeo yake waliondoka kwa kasi” alieleza Kamanda David Misime
Mkuu
huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya watu hao kuondoka kwa
kasi ndipo muuzaji huyo kugundua kwamba ameibiwa na kupiga simu Polisi
ambao waliwasiliana na vituo vyote vya mjini na nje ya mji na kufanikiwa
kuwakamata matapeli hao katika kituo/barrie ya Chanene liyopo wilayani
Chamwino pori la Mtungutu.
Kamanda
Misime aliwataja watuhumiwa hao waliokuwa wakitumia gari aina RAV 4 T.
872 CGE la rangi ya damu yam zee kuwa ni mwanamke Ahlam d/o Hassan,
miaka hamsini mwarabu na mkazi wa Tanga, mwanaume Daoud Esam@Abdelgawad ,
miaka 39 , msudani dereva na mkazi wa misri ambaye alikuwa na passport
ya kuiingia nchini tarehe 19/07/2013 na ana Visa ya kukaa Tanzania kwa
muda wa Miezi mitatu.
Wengine
ambao baada ya kuhojiwa, Kamanda alisema walikiri kufanya utapeli huo
ni Matata Laurence, miaka (38) dereva na mkazi wa Gongo la Mboto, Rahma
Mahamoud, miaka (26) Mkazi wa Dar es Salaam pamoja na Salehe Hamad
Mnene , miaka 40 na mkazi wa Manzese Dar es salaam.
Jeshi
la Polisi linatoa tahadhari kwa wanachi kuwa makini na ya watu
wanaofanya vitendo vya namna hii na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi
wanapotia shaka kwa watu wa aina hiyo, ili hatua za kuwadhibiti
zichukuliwe mapema.