Kesi ya
Bosco Ntaganda anayetuhumiwa kwa uhalifu wa kivita Katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo inaanza leo katika mahakama mjini The Heague
Uholanzi. Amekana madai ya kufanya uhalifu wa kivita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miaka kumi iliopita.
Bosco Ntaganda alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani nchini Rwanda mwaka uliopita wakati kundi lake M23 lilipoanza kulemewa.
Ni miongoni
mwa washukiwa wakuu wa ICC wanaotuhumiwa kwa kuwatumia watoto wadogo
kama wanajeshi,kuwatumia wanawake watumwa wa ngono na mauaji.
Kikao cha leo kinatarajiwa kuwasaidia majaji kuamua iwapo kuna ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka Ntaganda.
Chanzo - BBC Swahili