Baadhi
ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva ambao wanakwenda
kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta 2013,linalorajiwa kufanyika Agosti
17,kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma a.k.a Mwisho wa Reli
wakiwa kwenye kaburi la Msanii mwenzao,Marehemu Albert Mangwea mapema
leo asubuhi kwenye makaburi ya Kihonda,nje kidogo ya mji wa Morogoro,
walipokwenda kuzuru na kumuombea dua,walipokuwa wakielekea Mkoani
Kigoma.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen-





