Shilika
lisilo la kiserikali la support makete to self support SUMASESU
limezindua mradi wa miaka miwili wa mapambano ya maambukizi mapya ya
virusi vya ukimwi kwa vijana wenye umri wa kuanzia miaka kumi na tano
hadi ishirini na nne
Akizindua
mradi huo mkuu wa wilaya ya Makete Bi Josehine Matilo hapo juzi alisema
kuwa kuna vijana wengi mitaani ambao wanakosa shughuli za kufanya na
kuwataka kuunda vikundi vya ujasiliamali kwa kushirikiana na viongozi wa
maeneo husika sambamba kuvitumia vikundi hivyo katika shughuli za
uzalishaji ikwemo kilimo ili kuendana na kauli mbiu ya kilimo kwanza
ikilinganisha na ardhi ya makete kukubali kilimo cha mazao mbalimbali.
Pia bi
matilo amewataka viongozi wa ngazi ya kijiji kata hadi wakuu wa idara
ikiwa pamoja na idara ya afya kuonyesha ushirikiano wa kutosha kwa
shirika hilo katika utekelezaji hadi kufikia malengo ya wa mradi huo na
kukiri kuwa kuna baadhi ya miradi imekuwa ikishindwa kumalizika
kutokana na miradi hiyo kuachiwa mashirika pekee katika utekelezaji
Kwa
upande wake mkurugenzi wa shirika hilo bw.Egnatio Mtawa amessema kuwa
wataweka muda wa kupima utekelezaji wa mradi huo pamoja na uundaji wa
vikundi vya vijana na kuwaomba viongozi wa ngazi mbalimbali hasa maeneo
yanayotarajiwa kunufaika na mradi huo kwa kuonyesha ushirikiano kwenye
utekelezaji wa mradi huo
naomba
niahidi kitu kimoja kwamba tutaweka muda wa kupima utekelezaji wa mradi
kwamba siku ile tulielekeana hivi na utekelezaji umafikia na tumekutana
na changamoto hiziikiwa pamoja na uundaji wa vikundi naomba na serikali
katika baadhi ya sekta hasa watu wa afya alisema bw Mtawa
Aidha
kwa upande wake diwani wa kata ya Iniho ambaye pia ni makamu mwenekiti
wa halmashauri ya wilaya Bw Jison Mbalizi alisema kuwa katka kata tano
ambazo zinatarajia kunufaika na mradi huo ni zinatakiwa kiwa mfano wa
kuigwa katika mapambano ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na
kuahidi kwa upande wake konyesha ushirikiano pindi shirika hilo litakapo
wasili katika kata yake
Miongoni mwa kata ambazo zinatarajia kunufaika na mradi huo ni pamoja na Kitulo, Ipelele, Iwawa, Isapulano,na Iniho.




