Ofisa
Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda
akizungumza na waandishi wa habari jana kutoa takwimu za makusanyo ya
damu kwa mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu ambapo ulivuka malengo kwa
asilimia 111 kutoka chupa 36,278 mpaka 38,948. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Masoko na Uhusiano Bi. Rayah Hamad (Picha na Mpiga picha maalum).
==== ======== ======
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la
makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa
kukusanya chupa za damu 38,948 ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa
na chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka
Januari hadi Machi mwaka huu.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu Salama, Bw.
Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda inayongoza kwa
uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.
Alisema mafanikio hayo yametokana na uanzishajiwa
mpango wa damu salama wa kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari katika
jamii na kushirikisha wadau.
Bw. Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya wachangia Damu duniani
ambapo lengo la kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za
mpango wa Taifa wa damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla
ya chupa 8,683
Alisema Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi
za kiraia nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo vidogo vya kuchangia
damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma kutoka
chupa za damu 2,560 mpaka chupa3,151 kufikia Aprili hadi Juni
mwaka huu.
Aliwaomba wadau kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu
umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya
jamii na vipeperushi.
Bw.
Mwenda alisema ushirikiano ni
mdogo kati ya wahamasishaji wa Mpango wa damu salama na viongozi wa
Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya ya damu kidogo inayopatikana katika
hospitali zetu na miundo mbinu hafifu hususan barabara mbovu wakati wa ukusanyaji na
usambazaji wa damu.
Alisema
changamoto nyingine ni uuzwaji wa chupa
za damu kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si waaminifu
hivyo kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.
Bw. Mwenda
alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha
Mpango wa Taifa wa Damu Salama mwaka 2005 ili kuhakikisha uwepo wa damu salama
na ya kutosha kwa wote wanaohitaji.
Alisema shughuli za mpango ni pamoja na uhamasishaji
jamii kuhusu uchangiaji damu wa hiari, ukusanyaji upimaji na usambazaji wa damu
salama mahospitalini.
“Mpango wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi kwa
kushirikianana kitengo cha kuzuia magonjwa (CDC) na wadau wengine wa
Chama cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)”
alisema Bw. Mwenda.
Alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka lengo
la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika damu iliyokusanywa
asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili- Juni ikilinganishwa na asilimia 1.2 kipindi
cha Januari hadi Machi baada ya kujikita katika suala la uhamasishaji na kutoa
damu toka kwa jamii ambayo ni salama, kuboresha dodoso la wachangiam damu na
kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na wachangiaji
kujiepusha na tabia hatarishi ili wawe wachangiaji wa kujirudia.



