Afisa Uhusiano toka Mfuko wa Pensheni wa
PPF Lulu Mengele (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio ya mfuko na aina za mafao
ambazo mfuko inatoa kwa wanachama wake,
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.
Meneja Uratibu Ofisi za Kanda toka Mfuko
wa Pensheni wa PPF Mbarouk Magawa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu
ya namna mwanachama anavyoweza kupata taarifa mbalimbali za michango yake.
Meneja Uwekezaji toka Mfuko wa Pensheni wa
PPF Selestine Some akielezea mafanikio mbalimbali ambayo mfuko umepata tangu
kuanzishwa kwake miaka 35 iliyopita .
======= ========== ========
UTANGULIZI
Mfuko
wa Pensheni wa PPF ni Mfuko mkongwe hapa
nchini, ulianzishwa mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na.
372 kwa
madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena na hayo kwa wafanyakazi
wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.
majukumu ya mfuko
PPF ina majukumu yafuatayo:-
i)
kuandikisha
wanachama,
ii)
kukusanya
michango,
iii)
kuwekeza
michango inayokusanywa na
iv)
kulipa
mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo
kwa wanachama wake.
WIGO
WA UANACHAMA
Mfuko
unaandikisha wanachama kutoka katika sekta zote za uchumi mashirika ya umma,
makampuni binafsi, waliojiajiri wenyewe na sekta isiyo rasmi
Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba
baadhi ya mafao
ambayo Mfuko unatoa ni
- Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira.
Mpaka sasa PPF ina wastaafu wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni
3.7
Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi
tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.
- Mafao ya Ugonjwa
Hutolewa pale
ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na
imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena
- Mafao ya Elimu:
Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa
amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi.
Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi
4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014
Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita.
Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto
wanachama
UWEKEZAJI
Jukumu
linginge kubwa ni kuwekeza; Mfuko wa PPF unawekeza kwa mujibu wa sera ya
uwekezaji sambamba na mwongozo wa uwekezaji wa SSRA na BOT. Baadhi ya sehemu Mfuko unawekeza katika
·
Majengo kama vile ofisi
mfano PPF Tower,PPF Plaza Mwanza,vile vile wekeza kwenye hoteli,nyumba za
kupanga vile vile tume tumeshiriki kwenye ujenzi wa vyuo vikuu kama vile UDOM-kwenye
chuo cha Mifumo ya Komputa na chuo kikuu cha sayansi na Teknologia Nelson
Mandela kilichopo Mkoani Arusha.
·
Tumeshiriki kwenye
uwekezaji katika sekta ya Kilimo Kagera Sugar, 21st Century kiwanda
cha Nguo Morogoro
·
Uwekezaji mwingine ni
kwenye Mikopo ya Saccos kwa wanachama wetu ambapo PPF unakopesha wanachama
kwenye maeneo ya Kazi ambapo inasaidia kukuza uchumi
MAFANIKIO YA MFUKO
- Mfuko umetimiza miaka 35 mwaka huu na ulianza kwa mtaji wa shilingi million 50 mwaka 1992.lakini Mfuko unaendelea vizuri kwa kuwa na uwezo wa kulipa mafao kwa wakati bila kulazimika kuuza vitega uchumi au kukopa mahali popote
- Kwa upande wa thamani ya Mfuko:
Mfuko umeendelea kukua mwaka hadi mwaka ambapo kwa sasa
thamani ya Mfuko ni shilingi trillion 1.3
ukilinganisha na mwaka jana 2012 Desemba ambapo thamani ya Mfuko ilikuwa trillion 1.09
- IDADI YA WANACHAMA
Mfuko umeendelea kukua kwa upande wa uanachama ambapo
hadi kufikia mwezi Juni 2013, tulikuwa na jumla ya wanachama 224,193 ukilinganisha na wanachama 203,981 kwa mwezi Desemba 2012
- Matumizi ya mifumo ya habari:
Mfuko
umefanikiwa sana katika nyanja ya teknolojia kwa kuweza kulipa mafao kwa
kutumia mtandao, hivyo kulipa kwa wakati.
Vile
vile Mfuko umepunguza matumizi ya karatasi yaani ‘paper work’ kwa kurahisisha
malipo kwa wanachama na kwa upande wa watoa huduma tunatumia mfumo wa ‘E-banking’ yaani pesa zinatumwa moja
kwa moja kwenye akaunti ya mhusika.
Kupitia
mifumo ya kisasa ya PPF, mwanachama anaweza kupata taarifa zake za michango,
dai au pensheni kwa mstaafu kupitia simu ya kiganjani au tovuti ya Mfuko ambayo
ni www.ppftz.org
Mwanachama
anaandika neno michango anaacha nafasi anaweka namba ya uanachama
na kutuma kwenye namba 15553
Si
hivyo tu , bali hata mwajiri anaweza kupata taarifa za michango ya wafanyakazi
wake akiwa katika sehemu yake ya kazi bila kwenda katika ofisi za PPF hii
inaokoa muda na pia kuongeza uhakika wa uwasilishwaji wa michango ya wanachama.
Kwa
kutambua umuhimu wa matumizi ya mifumo ya habari mwaka huu 2013 katika wiki ya
Hifadhi ya Jamii, Mfuko wa Pensheni wa PPF ulitunukiwa hati ya utambuzi kama Mfuko bora kwenye matumizi ya
Mifumo ya habari. Hati hiyo ilitolewa na Mhe. Rais, Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete,kwa kuwa Mfuko bora katika Nyanja ya mifumo ya habari kwa kutumia
teknolojia ya kisasa kwenye kutoa huduma mbalimbali.
- Utoaji wa Mikopo ya SACCOS
PPF
ni waanzilishi wa mikopo ya SACCOS tulianza kutoa mikopo ya saccos mwaka 2004.
Tunatoa
mikopo hii kupitia SACCOS za wanachama wetu zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi.
Mpaka
sasa tumeshatoa zaidi ya Billioni 56 kwenye SACCOS 46
- Tuzo katika Utawala bora
Kwa
kutambua uwazi katika uendeshaji wa Mfuko Umoja Mifuko ya hifadhi ya Jamii
Duniani (issa) uliweza kutupatia Tuzo katika utawala bora kwa kuendesha
shughuli mbali mbali kwa uwazi kama vile mikutano ya wanachama na wadau PPF huu
ni mwaka wa 23 tuna desturi ya kukutana na wanachama na wadau wetu.
- Hati safi kutoka kwa CAG kwa kuwa na mahesabu yaliyo safi
- Uwekezaji ni mzuri ambapo tumewekeza katika sehemu mbalimbali kama vile hoteli za kitalii mfano East African Hotel Arusha na Gold Crest Mwanza ambapo watalii wengi wanafika hivyo inasaidia kwenye ukuaji wa Uchumi.
Tumewekeza
kwenye ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa ajili ya kuwauzia wanachama wetu.PPF
imekuwa Mfuko wa kwanza kwa kuanzisha miradi ya nyumba za bei nafuu.
Tulijenga
nyumba 580 Kiseke Mwanza na tuliziuza kwa bei nafuu ya kati ya shilingi millioni 16 mpaka million 33. Zoezi
hili ni endelevu kwa mikoa mingine
- Fao la Elimu:
PPF
imekuwa Mfuko wa kwanza kuwa na Fao la elimu kwa watoto wa wanachama
wetu.Ambapo lilianza kutolewa mwaka 2003 ambapo tangu tuanze kwasomesha kiasi
cha shilingi billion 3.6
LENGO
Katika
Mpango mkakati wa Mfuko kwa kipindi cha miaka 3 (2013-2015) baadhi ya malengo
ya Mfuko ni kama ifuatavyo:
Thamani ya Mfuko ni kukua kutoka trillion 1.09 Desemba 2012 na kufikia trillion 2 ifikapo Desemba
2015
- Na Idadi ya wanachama kuongezeka kutoka wanachama 203,981 Desemba 2012 kufikia laki 4 Desemba 2015.
Lengo
kuongeza mara mbili thamani ya Mfuko
Mwisho kabisa
ningependa kuwashukuru wanachama na wadau wote wa Mfuko kwa Mchango Mkubwa
Mliotupa
Hivyo tunaomba
tuendelee kushirikiana kwa kuendelea kuwa wanachama wa PPF na wale ambao bado
hamjajiunga na PPF tunaomba mjiunge ili muweze kuwa na uhakika wa maisha yenu
ya sasa na baadaye.
Asanteni
Lulu Mengele
Meneja Uhusiano na Masoko
Mfuko wa Pensheni wa PPF





