Kwa nchi kama Tanzania sio ajabu kabisa kushuhudia mtu akitupa
takataka kwenye mazingira ambayo hayaruhusu kabisa mfano yuko kwenye
gari inatembea anatupa chupa ya maji au uchafu mwingine wowote.. kuna
uwezekano hii picha ikabadilisha tabia ya mtu wa aina hii akiiona.
Huyu ni kunguru ambaye alionekana akiokota kopo la soda likiwa limezagaa na akaamua kuliokota na kuliweka mahali sahihi, kwenye ndoo maalum ya takataka… tufate mfano wake, kuna uwezekano kabisa ukiwa na uchafu ukaubeba mpaka sehemu maalum ya kutupa taka.