Rais Jakaya Kikwete (kushoto)
akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Sri Lanka hapa
nchini, Tahmbirajal Roveenthiran anayeiwakilisha nchi yake kutokea
Kenya. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam
Mwangalizi wa Ikulu, Shaban Gurumo
(kushoto) akimlaki Balozi mpya wa Thailand hapa nchini, Ittiporn
Boonpracong anayeiwakilisha nchi yake kutokea Nairobi Kenya. Hafla hiyo
kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Kikwete (hayupo
pichani) ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkuu wa
Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maharage
Juma
Rais Jakaya Kikwete (kushoto)
akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Ethiopia hapa
nchini, Shemsudia Roble anayeiwakilisha nchi yake kutokea Kenya
Bendi ya Polisi kipiga wimbo wa Taifa wa Tanzaniawakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete (kulia),
akizungumza na Balozi mpya wa Trinidad & Tobago, Patrick Edward
baada ya kupokea hati ya utambulisho. Anaiwakilisha nchi yake kutokea
Kampala, Uganda.



