Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Thursday, May 2, 2013

Ufafanuzi kuhusiana na Promotion ya uwindaji ya Serengeti Premium Lager


Kampuni ya bia ya Serengeti katika juhudi zake za kutambua na kuthamini wateja wake, leo imezindua promosheni ambayo inaendana na kampeni yake kuu inayoendelea ya TUPO PAMOJA.  Tupo Pamoja ni kampeni inayotambua wateja na kusherehekea nao pamoja.
Mteja anaweza kujishindia kuanzia shilingi elfu kumi hadi million moja na pia anaweza kujipatia bia ya bure papo hapo.  Kampeni hii inatarajiwa kuendeshwa kwa miezi mitatu ijayo.
Katika promosheni hii ya winda na ushinde, mteja atakaponunua bia ya  Serengeti ataweza kupata maelezo chini ya kizibo kama ilivyokuwa katika kampeni iliyopita ya vumbua hazi na chini ya kizibo.   Atapata namba maalum ambayo atatuma kwa njia ya sms kwa namba maalum na papo hapo atapata ujumbe utakaomjulisha ameshinda kiasi gani au kama amejipatia bia ya bure.   
Kama kawaida ili kuhakikisha ushindi huu ni waukweli na uhakika, promosheni hii itasimamiwa na bodi ya Bahati nasibu, kampuni maahiri ya PWC na itaendeshwa na Push Mobile.
Akiwakaribisha wageni na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuzindua promosheni hii ya Winda na Ushinde iliyofanyika katika kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru alisema kwamba bia ya Serengeti lager ni bia inayojali na kuwatambua wateja wake kwa kiasi kikubwa. 
“Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi.  Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
Uzinduzi wa promosheni hii pia ulihudhuri wa na Mkurugenzi mkuu (Group Managing Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.
Wengine waliohudhuria ni Maofisa kutoka bodi ya Bahati Nasibu, maofisawa PWC na Push Mobile.  Pia kutoa walihudhuria washindi waliowahi kushinda zawadi mbalimbali katika promoshen za nyuma.
 PICHANI JUU: Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Steve Gannon akionesha kizibo ya Serengeti Premium Lager chenye malekezo namna ya kujishindai zawadi mbalimbali, mbele ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo. 
Pichani kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na mmoja washindi aitwaye Rahma, aliyewahi kujishindia piki piki kupitia promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Bwa.Steve Gannon akionesha namna ya kutuma ujume wa promosheni ya WINDA NA USHINDE kwa kutuma ujumbe kupitia namba iliyowekwa maalum kwa promosheni hiyo,mbele ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na mmoja washindi aitwaye Rahma,aliyewahi kujishindia piki piki kupitia promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
 Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu “Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi.  Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
 Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu akifafanua zaidi kuhusiana na promosheni hiyo ya WINDA NA USHINDE iliyozinduliwa leo ndani ya kiwanda cha kampuni hiyo,Temeke jijini Dar na kuhudhuriwa na  Mkurugenzi mkuu (Group Managing Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.Shoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Steve Gannon.
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzindu wa promosheni hiyo mapema leo,wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Bwa.Steve Gannon alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu promosheni hiyo pia na pia kuwashukuru wateja wao wote ambao wamekuwa na wanaendelea kuwa nao.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...