Jana ilifanyika semina kwa wateule wa tunzo za muziki za Kilimanjaro za msimu huu ambapo kwa mara ya kwanza, wasanii walizipongeza kwa asilimia kubwa na kutoa maoni zaidi kuliko kuzikosoa kama ilivyokuwa awali.
Katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa New World Cinema maeneo ya Mwenge jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa pia na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa pia wasanii walipata elimu mbali mbali kuhusiana na jinsi mchakato mzima wa tunzo hizo utakavyokuwa ukiendelea.
Tunzo
za mwaka huu zimebeba jina la kivyetuvyetu zikiwahimiza watanzania
kupenda vya kwao, hamasa iliyowaingia wanamuziki hao ambao walionekana
kutoa mawazo ya kuboresha tunzo zaidi kuliko kuzitafuta makosa huku
wakiamini kwa asilimia mia moja kwamba hizi tunzo ni za kwao, na wana
jukumu la kuzifanya ziwe bora kwa kufanya nazo kazi bega kwa bega.
...katikati ni Nikkii wa pili kutoka kundi la Weusi
Kutoka kushoto ni Queen Darleen, mwasiti na Linah kutoka THT
Luiza Mbutu hapa akiwa katika utani na meneja wa Mashujaa Band, Martin Sospeter(Aliyevaa Tshirt Nyeupe)
george
Kvishe, meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini na
waendeshaji wa tunzo za za muziki Tanzania akiongea machache na wasanii
waliochaguliwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho mwaka huu
..mnh, ..huyu nae...
Linah, akiteta jambo na Rachel wakati mchakato ukiendelea
Mkubwa Fella, Meneja wa makundi ya THT na Mkubwa na wanawe akitoa mawazo yake katika semina hiyo
Malkia Khadija Kopa maye alipasha yake
meza kuu, ...(Bisha)
Jike la Simba, Isha Mashauzi naye alilonga yake
Nikki wa Pili naye alipata muda wa kutoa ya moyoni
Barnabas kutoka THT
Rama Dee
Linex