Shaban Waziri- Katibu msaidizi wa Soko la Mashine tatu akizungumzia kero hiyo.
Jafari Sewando- Mwenyekiti wa Soko la Mashine tatu akizungumzia hatua ya wafanyabiashara kugomea kulipa ushuru.
Mfanyabiashara (mama Elia) akiwa anasubiri wateja katika eneo lake la biashara.
Ramadhan Waziri akitoa kero dhidi ya wenzao kuuza bidhaa nje ya Soko hilo na wao kukosa wateja.
LILE
sokomoko la wafanyabiashara wa soko la Mashinetatu Mkoani Iringa
limechukua sura mpya baada ya wajasiriamali wanaoendesha biashara zao
ndani ya soiko hilo kugomea kulipa ushuru mkoani Iringa wamegoma kulipa
-kwa madai ya kuwa wanapata hasara kwa kuwakosa wateja baada ya manispaa
kushindwa kuwabana wafanyabiashara wanaouza nje ya masoko rasmi
yaliyotengwa, na hivyo Manispaa kupoteza zaidi ya sh. 2.5 zinazokusanywa
kwa mwezi sokoni hapo.
Wakizungumzia
hatua ya wao kufanya hivyo, wafanyabiashara hao wamesema hawaoni sababu
ya kulipa ushuru wa soko hilo wakati mali zao zinaoza kila siku kwa
kukosa wateja, baada ya wafanyabiashara wenzao kupanga bidhaa nje ya
soko hilo na hivyo wateja kushindwa kuingia ndani ya soko.
"Sisi
hatulipi ushuru, kwa sababu wenzetu wanaowadaka wateja huko nje
barabara hawalipi ushuru, sie ambao tunaozesha tu mali zetu kwa kukosa
wateja ndiyo tunalipa huo ushuru, sasa kuanzia leo hatutoi ushuru,"
Alisema Ramadhan Waziri.
Lucy
Kifalu na Sofia Hello wamesema bidhaa zao kama Nyanya, Vitunguu na
mbogamboga zimekuwa zikioza, na hivyo mitaji yao kukatika kila siku
baada ya wenzao kufanya biashara katika eneo la barabara na hivyo wateja
kushindwa kutoingia katika soko hilo.
Juliana
Sanga amesema hata mikopo ya fedha waliyochukua katika benki ili
kuendeshea biashara zao wanashindwa kurejesha, na hivyo kuwa katika
hatari ya kunyang'anywa mali zao.
"Hapa
tulipo tunamikopo, tulikopa kwa ajili ya kuzungusha mtaji wa biashara,
lakini kutokana na hali hii ya wengine kufanya biashara nje ya soko
hili, tena barabarani, kwa hiyo wateja hawaji humu sokoni, wanaishi huko
nje, kwa hiyo sisi hatulipi ushuru mpaka wawaondoe wale wanaowadaka
wateja pale nje," Alisema Juliana.
Ramadhan
Nasoro na Maulisia Mbilinyi nao wakasema kutokana na kudolora kwa
biashara sokoni hapo, wanashindwa hata kurejesha madeni ya mikopo ya
fedha waliyokopa katika taasisi za kibenki, kutokana na biashara zao
kukosa soko.
Aidha
ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kupitia mwanasheria wake,
Innocent Kihaga amesema wataendesha zoezi la kuwakamata wale wote
wanaokiuka sheria za masoko ya manispaa hiyo.