
Mjumbe
maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu
Mary Robinson amesema mkataba wa hivi maajuzi wa amani unaojumuisha nchi
11 za ukanda huo umeonyesha uwepo wa matumaini ya kufikia amani katika
eneo hilo.
Mary
Robinson ambae ni rais wa Jamhuri ya Ireland ameyasema hayo jana wakati
wa ziara yake jijini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
na kaongeza kuwa Suluhu la mgogoro wa eneo hilo itapatikana kutokana na
mchango wa pande zote husika na mgogoro huo.Katika mazungumzo yake na
Gavava Julien Paluku Kahongya, Robinson alisema kuwa amesikia mengi,
ambayo atafanyia kazi mapema ili kuondoa hali ya wasiwasi na ukosefu wa
usalama huko mashariki mwa DRC.
Kwa
Upande wake Gavana wa Mkoa wa Kivu ya Kaskazini Julien Paluku pamoja na
kuridhika na ziara hiyo, amesema kuwa kuna matumaini ya kufikia amani ya
kudumu katika eneo hilo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.
Kabla ya
kuondoka Mkuuhuyo alisema ataomba msaada wa jumla kwa mashirika ya
kiraia, mashirika ya wanawake, vijana na makundi ya kidini ya kanda hii
kushawishi serikali zao kuhusu utekelezwaji wa mkataba wa Addis Ababa.
Katika
hatua nyinge hii leo kiongozi huyo anatarajiwa kuwasili nchini Rwanda
baada ya kumaliza ziara yake huko DRC ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake
katika kanda hii.