Kundi lenye siasa kali la Al-Shabaab la Somalia limetangaza kuhusiana na
shambulizi la bomu la kujiua lililotokea leo asubuhi mjini Mogadishu,
na kusababisha vifo vya watu 10.
Chombo cha habari cha taifa cha Somalia kimesema, shambulizi hilo lililenga msafara wa magari ya serikali ya Somalia yaliyowabeba maofisa wa Qatar, ambao hawakujeruhiwa katika tukio hilo.
Gari la waziri wa ndani wa Somalia pia lilikuwa miongoni mwa msafara huo, lakini waziri mwenyewe hakuwemo katika gari.
Tukio hilo limetokea leo asubuhi wakati mshambuliaji wa kujiua akiendesha gari lililobeba mabomu kugongana na msafara wa magari ya serikali karibu na kituo cha mabasi K4 mjini Mogadishu.
Shambulizi hilo limekuja siku moja tu baada ya serikali ya Somalia kuondoa hatua kali za usalama zilizodumu kwa siku nne katika barabara muhimu karibu na ofisi za serikali.
Tovuti moja inayounga mkono Al-Shabaab imewakariri makamanda wa kundi hilo wakisema wapiganaji wa kundi hilo wanahusiana na tukio hilo, na kuapa kufanya mashambulizi mengi zaidi.