Serikali ya Afrika Kusini imekanusha ripoti za vyombo vya habari kuhusu
kutekwa nyara kwa raia 12 wa nchi hiyo wanaofanya kazi ya kutegua mabomu
ya ardhini nchini Senegal.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini Clayson Monyela, amesema habari hizo si za kweli.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, watu hao 12 kutoka kampuni ya kutegua mabomu ya Mechem ya Afrika Kusini walitekwa nyara huko Casamance, sehemu ambayo wapiganaji wa kundi la Movement of Democratic Forces of Casamance MFDC wamekuwa wakipigania kujitenga na Senegal toka mwaka 1982.
Fred Weyers ambaye ni mkurugenzi wa tawi la kampuni ya Mechem nchini Senegal, aliambia shirika la habari la Senegal kwamba, wafanyakazi 12 wa kampuni hiyo hawajulikani walipo tokea Ijumaa, na inaaminika kuwa, wanashikiliwa na waasi wa kundi la MFDC.