BUNGE la Jamhuri la Muungano
wa Tanzania limeonekana kuwachosha baadhi ya wasanii kutokana na kukosa
hoja za maana za kujadili ndani ya bunge hilo na matokeo yake kuwa kama
kijiwe kwa kutumia lugha chafu zilizokosa tija kwa taifa
Kutokana na hali hiyo ya
baadhi ya wabunge kukosa lugha na sera zenye tija wawapo bungeni baadhi
ya wasanii wanaliona hilo ni moja ya changamoto inayosababisha
watanzania kuzidi kuwa na hari ngumu ya kimaisha kwa kukosa watetezi
wenye umakini
Mmoja wa wasanii hao
akizungumza na jarida hili Ben Pol alisema kuwa anashangazwa na baadhi
ya wabunge kutumia lugha ya matusi kwenye kujadili hoja na matokeo yake
wanashindwa kupata muafaka wa wanayo yajadili
Alisema kuwa bunge limekosa
muelekeo na ameacha kulisikiliza bunge hilo kwa sababu ya kukosa mueleko
na kujaa lugha chafu za matusi huku wakishindwa kuyajadili yale ya
msingi kwa taifa lao
Kutokana na hali hiyo nchi ya
Tanzania itaendelea kubaki maskini na vitu kuendelea kupanda bei kila
siku huku kipato cha wananchi kuwa duni kwa kukosa watetezi
Alisema kuwa bunge halijafika
sehemu nzuri na kuonekana halina tija kwa wananchi wake na hali hiyo
linasababisha wananchi kushindwa kupata ukombozi kwa yale
wanayoyakusudiwa
Kwa upande wake msanii wa
filamu nchini Rose Ndauka alisema kuwa bunge limekuwa si la wastaarabu
na matokeo yake wanajadili vitu ambavyo havina tija kwa jamii
Alisema kuwa Tanzania ni
nchini ya wastaarabu na wajadili vitu vya ustaarabu kwa kufikia muafaka
hali hiyo imekuwa tofauti sasa kwa baadhi ya wabunge kujadili vitu kwa
lugha chafu hali inayoshangaza taifa
"Wananchi tumewachagua wabunge
huku tukiamini kuwa watafanya hilo tulilowaagiza ila hali imekuwa
tofauti na mika mingine baadhi ya wabunge kuanza kujadili vitu visivyo
na tija kwa wananchi wao" alisema Ndauka