Mwanamuziki toka
mkoani Morogoro anayefanya poa kwa sasa na wimbo wake wa Leo
mwanadada Dayna Nyange a.k.a Mkali wao, amefunguka na kumpigia
saluti mwanamuziki mkongwe toka hapa Morogoro Afande Sele.
Akiongea na ubalozini.blogspot.com
toka jijini Mwanza aliko sasa katika ziara ya kimuziki na
uzinduzi wa Albam ya Kala. Dayna amesema huwa anamkubali afande
kwa tungo zake
'' kwa kweli siku
zote, nimekuwa nikimkubali sana Afande sele kwa tungo zake
zenye ujumbe, lakini kwa wimbo huu wa Dini tumeletewa, nampigia
saluti. Afande ni bonge la msanii na huwa naskiliza nyimbo zake
kwani najuwa nikiskiliza nyimbo zake kuna madini napata, lakini
sasa kaka mkubwa kwa hapa alipofikia na kufikilia kwa kina juu
ya wimbo huu, anastahili kuwa mfalme wa Rhyme, waliompa tuzo
hawakukosea. Big up sana Afande, saluti kwake, aendelee kuwa
mwalimu wa ujumbe , huuwimbo ni zaidi ya Hotuba ya kitaifa
Inayotolewa na Rais''
Amesema Dayna