
Akizungumza
na Vyombo vya Habari Mkurugezi wa Kampuni ya datk Intertaimeint, Asha
Kigundula alisema kwa maandalizi ya shindano hilo ndiyo yanaanza na
kutaka warembo wajitokeza kushiriki.
Asha
alisema fomu zitapatikana katika ofisi ya Mwananchi iliyopo bandari
Tanga gorofa ya Nne, Five brathers kwa nassa makau iliyopo jijini humo,
kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo jingo
la Hifadhi Hause Posta.
“Mazoezi
kwa warembo yataanza ijumaa ya Mei 3 mwaka huu jijini Tanga, warembo
hao watakuwa chini ya walimu wawili ikiwa ni pamoja na mshindi wa mwaka
jana wa mkoa huo Teresia Kimolo”alisema Asha.
Alisema
kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani
humo kwa kuwa Kampuni datk imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya
urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.