Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo.
Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa
kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe
na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.