
Aliyekuwa
Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Murro,akiwa
chini ya ulinzi wa Asakari Polisi Dar es Salaam,Tanzania
MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam kesho inatarajia kutoa uamuzi wa mgumu
utakaowezesha kesi ya aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili kudiwa umpya ama kusitishwa.
Muro na
wenzake wawili, Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’ na Deogratius
Mugassa wanaweza kupandishwa kizimbani tena na kuanza kusikiliza upya
kesi ya rushwa iliyokuwa ikiwakabili.
Kwa
muujibu wa taarifa za ndani kutoka Mahakama ya rufaa zilizonaswa
naHabaimpya.com ni kwamba Uamuzi huo unatokana na maombi ya Jamhuri
katika rufaa ya kupinga hokumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
iliyowaachia huru Muro na
Ikiwa Mahakama Kuu itakubaliana na hoja na maombi ya Jamhuri, basi Muro na wenzake watalazimika kupanda kizimbani tena katika
Mahakama ya Kisutu na kesi yao itaanza kusikiliza upya, kama vile ilikuwa haijawahi kusikilizwa kabisa.
Jamhuri
itaibidi iwaite tena mashahidhi wake kufika mahakamani kutoa ushahidi na
kama mahakama itaridhika kuwa washtakiwa hao wana kesi ya
kujibu, basi watalazimika kujitetea na hata kuwaita mashahidi wao kama watakuwa nao, kisha mahakama itatoa hukumu yake.
Kama
Mahakama Kuu haitakubaliana na hoja na maombi ya Jamhuri, basi itaweza
kuamuru usikilizwaji wa rufaa hiyo uendelee ambapo Jamhuri
itaendelea
na hoja zake nyingine za kupinga hukumu ya sasa ya Mahakama ya Kisutu.
Muro na wenzake, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama na
kuomba rushwa ya Sh10 milioni, kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage.
Hata hivyo
Novemba 30, 2011, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Frank Moshi katika
hukumu yake, aliwaachia huru, akisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa
kuthibitisha mashtaka dhidi yao bila kuacha mashaka yoyote. Jamhuri kwa
kutokuridhika na hukumu hiyo, ilikata rufaa Mahakama Kuu, ikibainisha
sababu nne za kuipinga hukumu hiyo.Rufaa hiyo ilisikilizwa na Jaji Dk
Fauz Twaib.