Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, April 29, 2013

Chuo cha kwanza cha confucious nchini Tanzania chazinduliwa


Chuo cha confucious cha chuo kikuu cha Dodoma, ambacho ni chuo cha kwanza cha confucious nchini Tanzania, kimezinduliwa jana mjini Dodoma. 

Chuo hicho kinachopewa jina la mwanafalsafa maarufu wa kale wa China, Confucious, kinabeba majukumu ya kueneza lugha ya Kichina na kuimarisha mawasiliano ya tamaduni za China na nchi nyingine. 

Vyuo vingi kama hicho vimeanzishwa katika nchi nyingi duniani, zikiwemo Kenya na Uganda katika kanda ya Afrika Mashariki. 

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na makamu wa rais wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal, waziri wa elimu wa nchi hiyo Bw. Shukuru Jumanne Kawambwa, na balozi wa China nchini humo Bw. Lu Youqing . 

Akihutubia wakati wa hafla hiyo, Dr. Bilal alisema, Tanzania na China zina historia ndefu ya ushirikiano ambao umewanufaisha wananchi wa pande zote mbili. 

Kuanzishwa kwa chuo cha confucious nchini Tanzania ni moja ya mikakati ya kuimarisha ushirikiano huo, na kutasaidia kuimarisha na kusukuma mbele zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili. 

Balozi Lu Youqing amepongeza kuanzishwa kwa chuo hicho ni fursa muhimu ya kuimarisha mawasiliano na kuongeza maelewano kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...