Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, April 29, 2013

BG TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUIFIKIA JAMII NA WAAJIRIWA


DSC_0594 
Mshauri wa Maswala ya afya wa Kampuni BG Tanzania Dk John Wijnberg (Kulia) akikabidhi msaada wa regulator na oxygen administration blocks kwa Mratibu tiba wa Hospitali ya Mwananyamala Dk Delila Moshi(kushoto) na Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Kariamel John jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani mwishoni mwa wiki, BG Tanzania iliandaa matukio mbali mbali Dar es Salaam na kwingineko Tanzania. Hii ilikuwa ni pamoja na kuisaidia hospitali ya Mwananyamala; mafunzo kwa waajiriwa kuhusu uzuiaji wa malaria; kuchangia vyadarua kwa waajiriwa na wenye mikataba; na mafunzo kuhusu malaria. Mafunzo haya yalijumuisha maelekezo ya  kivitendo kuhusu namna ya kutumia vifaa vya kupima ugonjwa huo kwa haraka.
 Dr. John Wijnberg, mshauri wa kiafya wa BG, alieleza jinsi kampuni hiyo inavyotia bidii katika jitihada za kupambana na malaria. “Usalama ni wa muhimu katika mafanikio ya operesheni zetu, ambazo zinategemea pakubwa rasilimalikazi  yenye afya, ari na iliyo katika hali nzuri. BG Tanzania inachukulia malaria kama mojawapo ya majanga makubwa dhidi ya afya kwa rasilimali yake ya thamani zaidi, waajiriwa, na familia zao,” alisema Dr Wijnberg.
 “Kwa mantiki hiyo, BG Tanzania imebuni mpango mathubuti wa kusimamia malaria ndani ya rasilimali za BG Tanzania kwa ajili ya kushughulikia maeneo yote muhimu ya kuthibiti malaria, na imeweka lengo lake la kiafya la mwaka kuwa ni uwepo wa matukio sifuri ya malaria,” aliedelea kusema.
 BG Tanzania hivi karibuni iliungana na mradi wa malaria wa United Against  Malaria wa Chuo Kikuu cha John Hopkins, na sasa tumekuwa kampuni yenye furaha iliyo salama dhidi ya malaria. Kuwa kampuni salama dhidi ya malaria, inajumuisha kusimamia mihimili minne ambayo kampuni zilizo salama dhidi ya malaria zinatakiwa kufanyia kazi ambazo ni: elimu, ulinzi, utetezi na kutambulika/uwazi. Kwa kufuata hatua stahiki, kampuni inapunguza hatari ya malaria kwa wafanyakazi wake wote, familia zao na jamii ya karibu.
 Kama mojawapo ya jitihada hizi na kwa ajili ya siku ya malaria duniani, Dr. Wijnberg alitoa maelezo kuhusu uelewa wake juu ya kutibu malaria kwa manesi waajiriwa  waliopo mstari wa mbele katika wodi ya masuala ya watoto katika Hospitali ya Mwananyamala. Wakati wa kazi hii BG ilichangia vifaa viwili vya uthibiti na vile vya kumpa mtu hewa ya oxigen pamoja na kusaidia kununua mitungi mipya miwili ya hewa ya oksijen. Vifaa hivi ni muhimu kwani tiba ya oxijen ni nyeti sana katika kuwatibu wagonjwa walio katika hali mbaya.
 Baadaye siku hiyo, Dr.  Wijnberg aliongoza mafunzo ya kujenga uelewa kwa waajiriwa wa BG Tanzania katika makao yake makuu yaliyopo Masaki,   Dar es Salaam. Mafunzo ya aina hiyo pia yalifanyika kwa makandarasi wa BG Tanzania mchana huo.
  “Kuwa katika usalama dhidi ya malaria, kunadhihirisha jithada za BG Tanzania za kusaidia jithada zote za kupambana na ugonjwa huo ndani ya kampuni,” Dr. Wijnber alieleza
 Kwingineko nchini, BG Tanzania ilifanya mazungumzo ya kujenga uelewa na ikagawa vyandaru vilivyotibiwa kwa dawa za wadudu kwa waajiriwa na makandarasi katika sehemu zao za kazi Mtwara pamoja na wafanyakazi wanaofanya kazi baharini katika vituo vya uchimbaji mafuta.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...