Steven-Monjeza-and-Tiwong-001
Raia wawili nchini Malawi wanaotuhumiwa kuendesha ndoa ya jinsia moja wakiwa chini ya Ulinzi. (Picha na Maktaba).
Wakili mmoja wa Umoja wa Ulaya amependekeza mashoga kutoka nchi ambazo sheria zao zinayachukulia mahusiano ya watu wa jinsia moja kuwa  haramu, kwamba wanapaswa kupewa hifadhi.
Wakili Eleanor Sharpston alikuwa akizungumza katika kesi ambayo wanaume watatu kutoka Sierra Leone, Uganda na Senegal walinyimwa hadhi ya wakimbizi nchini Uholanzi.
Serikali ya Uholanzi imesema wanaume hao wangekuwa na miendo ya kujizuia katika nchi zao.
Sharpston amepinga hoja hiyo akisema mashoga wanapaswa kupewa hadhi ya wakimbizi iwapo wataweza kuthibitisha wameteswa.
Watu wengi wa jinsia moja walio katika mahusiano ya kimapenzi  wanaoishi barani Afrika, wanakabiliwa na kutengwa na mateso.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema ushoga ni hatia katika nchi 38 za Afrika.