DSC00179 (4)
Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP.Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha),juu ya kukamatwa kwa vijana watano wanaojihusisha na uuzaji wa Bhangi.Vijana wamekamatwa na bhangi misokoto 927 yenye uzito wa gram 462.(Picha na Nathaniel Limu).
**********
Na Nathaniel Limu.
Jeshi la polisi mkoa wa Singida linawashikilia vijana watano kwa tuhuma ya kumiliki madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 927 yenye uzito wa gramu 462 wakiwa kwenye harakati ya kuyauza.
Kamanda polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema vijana hao wamekamatwa kufuatia operesheni kali inayoendelea maeneo mbalimbali mkoani Singi,kusaka wahalifu.
Amesema John Stephano (17) na Dina Rokasi (17) wote wakazi wa kijiji cha Kipondoda wilaya ya Manyoni, wamekamatwa wakiwa na misokoto 731 ya bhangi yenye uzito wa gramu 365.
Kamwela amesema watuhumiwa hao walikutwa na bhangi hiyo baada ya kupekuliwa nyumbani kwao kutokana na taarifa za raia wema.
Aidha, almeema Kaiza Patrick (28) mkazi wa Mwenge na Idd Hassa (28) mkazi wa Ipembe mjini Singida wamekamatwa na misokoto 13 yenye uzito wa gramu sita wakiwa wanaiuza katika maeneo ya uwanja wa michezo wa Namfua.