Ni kama miujiza kwa mtoto wa kichina kuwa hai mpaka sasa licha ya
kuchomwa chomwa mara 90 na mama yake mzazi huko China kwa madai kuwa
alimng’ata ziwa mama yake wakati akinyonyeshwa.
Kwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye miezi 8 tu ameshonwa
zaidi ya nyuzi 100 ili kuurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya
shambulizi hilo lililotokea katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China.
Bao anaishi na mama yake pamoja na wajomba zake wawili ambao
wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwaajili ya kipato. Mmoja wa
wajomba hao ndiye aliyegundua kuwa Bao ameumizwa baada ya kumkuta akiwa
amelala kwenye damu iliyotapakaa nyumbani hapo kabla hajamkimbiza
hospitali.
Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kumchoma choma mwanae na mkasi mara
90 hususan eneo la usoni baada ya mtoto huyo kumng’ata ziwa wakati
akimnyonyesha.
Baada ya tukio hilo majirani wa familia hiyo wameiomba serikali
imnyang’anye mama huyo wa kichina mtoto kwa sababu za kiusalama, lakini
ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa hakuna uthibitisho wowote mpaka
sasa kama mwanamke huyo anamatatizo ya akili, lakini wameongeza kuwa
hata hivyo mtoto huyo bado ana walezi wengine wawili anaoishi nao
(wajomba zake) Mtoto huyo anaendelea kupata nafuu akiwa hospitali.