Na Richard Bukos
OPARESHENI
Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na mapaparazi wa Global Publishers
inazidi kufichua ‘madudu’ kwenye jamii, safari hii imekutana na machangu
ambao wamecharuka kuendeleza biashara hiyo kwa kisingizio cha kutafuta
fedha za kununulia futari.
‘Askari’
wa OFM, wiki iliyopita alifanya uchunguzi katika viunga mbalimbali
maarufu kwa biashara hiyo na kukuta machangudoa wakifanya biashara yao
kama inavyokuwa katika miezi ya kawaida.
Maeneo
ambayo yalionekana kushamiri zaidi kwa biashara hiyo ni Barabara ya
Mwananyamala Hospitali, American Chipsi, Makaburi ya Kinondoni, Viwanja
vya Leaders Club, Taasisi ya Moyo, Jolly Club (Masaki), Hospitali ya
Agha-Khan, New Maisha Club (Masaki) na Coco Beach. NA GPL
Idadi
kubwa ya wadada hao walipohojiwa na paparazi wetu, walisema wanaendelea
na biashara hiyo kwa kuwa ndiyo waliyoizoea kutafutia kipato na
wakiiacha, watakufa kwa njaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan.
Ili
kujiridhisha kwa data, paparazi wetu alijifanya mteja na kukutana na
machangu wa Makaburi ya Kinondoni ambao walidai wanapenda waitwe
‘scraper’ au vyuma chakavu pasipo kufafanua zaidi, bahati mbaya
wakashtukia mchezo:
Changudoa:
“We kaka mbona unatuzingua? We ulivyokuja si ulijifanya mteja, kumbe
paparazi, sisi hatuwezi kuacha kujiuza kwa kuwa ndiyo kazi tuliyoizoea,
sasa tukikaa nyumbani tutapata wapi futari?” alihoji mmoja wa
machangudoa.
Paparazi: “Hivi ni kweli nyie mnafunga?”
Changudoa:
“Wewe tumia ubongo na maswali yako yanayotia njaa, hata kama sisi
tunafunga au hatufungi tuna watu wanaotutegemea majumbani kwetu
kuwatafutia futari, sasa tusipohangaika itakuwaje?”
Baadhi ya
waumini wa dini ya Kiislamu waliozungumza na Ijumaa Wikienda,
walionesha kukerwa na tabia hiyo na kulaani vibaya kwani mwezi huu ni
maalum kwa ajili ya kumrudia mwenyezi Mungu na kuacha dhambi.