Picha mbalimbali zikionesha utekelezwaji wa adhabu ya kukatwa vidole mhalifu. |
Imepigwa
picha kwa mara ya kwanza kabisa, hiki ni chombo cha kinyama
kinachotumiwa na mamlaka za Iran kukata vidole vya wahalifu wenye hatia.
Wanaume
watatu wenye skafu wanaoneshwa wakitumia mashine chafu ya kusagia
kutekeleza adhabu hiyo ya kikatili, iliyotolewa chini ya sheria kali
nchini humo ya Sharia, dhidi ya mwizi aliyepatikana na hatia na mbakaji.
Mwanaume
huyo aliyefunikwa macho, ambaye alipatikana na hatia katika mahakama
huko mji wa kusini-magharibi wa Shiraz, anaonekana akiongozwa kuelekea
kwenye chombo hicho, ambacho kinaweza kuwa kimechukuliwa kutoka katika
duka la mbao.
Wanaume watatu wenye skafu kisha wakamvuta mtu huyo na mkono wake kufungwa sehemu inayotakiwa kwenye mashine hiyo.
Huku mtu
mmoja akiendesha gurudumu, mashine hiyo ya kikatili inafanya kazi yake
na kisha mkono wa mtu huyo unainuliwa kuonesha damu inayochuruzika kabla
ambao baadaye unatumbukizwa kwenye madini joto ghafi.
Katika
namna ya ajabu sura ya mtu huyo inaonesha kutohisi maumivu kushawishi
kwamba inawezekana alinyweshwa dawa au kupewa ganzi kabla ya mchakato
huo.
Kufuatia ukataji viungo huo, mwendesha mashitaka alitangaza kwamba adhabu za uhalifu kama hizi zinaweza kuwa kali zaidi.
Chini ya
sheria za Sharia, ukataji viungo, kuchapwa mijeledi, na pengine kifo kwa
kupigwa mawe zote ni aina ya hukumu za kisheria.
Picha
hizi zilisambazwa na shirika la habari la nchi hiyo huku Iran ikijiandaa
kuelekea kwenye uchaguzi mwezi Juni kumbadili Rais Mahmoud Ahmadinejad
ambaye atakuwa ametumikia kwa kipindi chake cha mwisho cha awamu mbili.