Ma Ailun ... in flight attendant uniform |
Inarepotiwa
kwamba kampuni ya APPLE watengenezaji wa simu aina ya iPhone 5 wameanza
uchunguzi baada ya maisha ya mwanadada mrembo pichani kukatishwa na
kichao daiwa shoti ya umeme iliyo tokana na simu yake aina ya iPhone 5.
Ma
Ailun, 23, alipatwa na shoti ya umeme wakati akijibu simu yake ikiwa
kwenye charge inarepotiwa. Ajali hiyo mbaya hadi kufikia kupoteza maisha
ya mrembo huyo ilitokea Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Xinjiang
Province nchini China.
Mrembo
huyu ambaye alikuwa muhudumu wa kwenye shirika la ndege la China
Sourthern Airlines na kuacha kazi hiyo hivi karibuni alinunua simu hiyo
mwezi Desemba kweney duka la Apple nchini humo na alikuwa anatumia
charger halisi ya Apple pia familia yake inareport.
Kaka yake amesema simu hiyo pamoja na charger yake vimekabidhiwa polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mzungumzaji wa kampuni ya Apple amesema: "Tunasikitishwa
sana na tukio lilitokea na tuanatoa pole kwa familia ya Ma Ailun.
Tutachunguza kwa kina na kushirikaina kikamilifu katika uchungunguzi wa
jambo hili."
Tukio
hilo limewapa wasiwasi watumiaji wa simu hiyo huku wataalam huko Hong
Kong wakionya watu kuto tumia vifaa vyovyote vya umeme vikiwa kwenye
charge (umeme).
Johnny Sin Kin-on, profesa katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia kilichopo Hong Kong amesema: "Kuna hatari ya kutumia kifaa cha umeme chenye betri wakati kikiwa kwenye charge (umeme), iwe shaver (kinyoleo) au simu."
Simu
aina ya iPhone 5 imekuwa imekuwa ikipokea malamiko mengi toka iingie
sokoni kutoka kwa wateja wake. Malalamiko yalikuwa pamoja na ubunifu
(utengenezaji) wake kutokuwa mzuri, charger yake pamoja na apps yake ya
rami kutokuwa na ufasaha.
Wiki
iliyopita iPhone 5 ilionekana kuwa ni simu ambayo imepoteza umaarufu na
mauzo yake kushuka sana nchini Uingereza. Na katika test za Benchmark
pia imeonekana kuwa na NUSU ya speed, ukilinganisha na simu aina ya
Samsung Galaxy S4 ambayo kwa sasa iko juu sana.
Credit: Jestina-George.com,