Jimmy Master
YULE
muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa na
mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya tatu na
baadaye kujiongezea jina lingine akiitwa J Plus.
Kwa
sasa nyota huyo amefunguka kuwa yukombioni kutoa muvi ya
mwisho inayoitwa Doble J Final huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka
baada ya kutangulia na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka
mwaka jana.
"Mwaka
jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu
hususani wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya
kipelelezi,"alisema J Plus.
Alisema
Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na kuna
heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika
kuonesha ubabe
wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unao tazamiwa kuingia sokoni
mapema tu , mwezi ujao .
Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine
katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy' na pia wamo nyota
wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na
Veronica Viankero.



