Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Mwema
|
Na Esther Macha, Mbeya
ASKARI
Polisi wa Kikosi cha FFU Mkoani Mbeya aitwaye G.9386 Pc Patrick(23)
amefariki dunia baada ya kugongwa na gari eneo la Benki kuu Jijini hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana , Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Bw.Diwani
Athuman alisema kuwa tukio hilo limetokea juni 23 mwaka huu.
Kamanda
Diwani alisema kuwa gari na dereva asiyefahamika, liligonga gari T.741
BXU aina ya March lililokuwa limeegeshwa eneo la hilo kisha kumgonga
mtembea kwa miguu askari Polisi aitwaye EX.G 9386 PC Patrick(23) na
kusababisha kifo chake papo hapo.
‘’Chanzo
kinachunguzwa dereva alikimbia na gari mara baada ya tukio na mwili wa
marehemu umesafirishwa kwenda Dodoma kwa ajili ya mazishi na yeyote
mwenye taarifa za alipo dereva huyo na gari atoe taarifa kwenye mamlaka
husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake’’alisema.
Wakat huo
huo, nyumba ya vyumba 12, mali ya Teresia Mwaijibe(40), iliungua kwa
moto na kuunguza vyumba 10 vya nyumba hiyo eneo la Mlima reli mjini
Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini.Kama
Kamanda Diwani amesema kuwa moto
huo ulizimwa kwa ushirikiano wa wananchi, polisi na jeshi la zima moto
na hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliyotokea katika ajali hiyo ya
moto.




