ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama
kisiwani Pemba, wakiwa katika zoezi la kuokoa miili ya Marehemu
waliopoteza maisha katika ajali ya kuangukiwa na Ukuta wa tangi la Maji
Machomanne Chake Chake Pemba leo
Askari wa JWTZ, kwa kushirikiana na
Askari wa vikosi vya SMZ, wakiingiza miili ya marehemu iliyoangukiwa na
ukuta wa tangi la Maji Machomanne, katika gari ya kubebea wagonja
Ambalesi kwa kuipeleka katika hospitali ya Chake Chake
ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama
kisiwani Pemba, wakiutoa mwili wa Marehemu juu ya Mnara wa tangi la Maji
Machomanne, ulioangukiwa na ukuta wa tangi hoo
WANANCHI mbali mbali wakiuangalia mnara
wa Tangi la Maji Machomanne, ulioanguka na kupoteza maisha ya wananchi
watatu leo asubuhi. (picha na Abdi Suleiman
ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama
kisiwani Pemba, wakiupeleka mwili wa marehemu katika gari ya kubebea
wagonja, ulioelemewa na ukuta wa mnara wa Tangi la Maji Machomanne Pemba
WANANCHI mbali mbali wakiwa katika
hospitali ya chake chake , wakitizama miili ya ndugu zao waliopoteza
maisha baada ya kuangukiwa na mnara wa tangi la maji Machomanne Pemba
Mkuu wa mkao wa kusini Pemba, Juma
Kassim Tindwa, akimfahamisha jambo waziri wa Nnchi Ofisi ya Makamo wa
Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, walipofika katika Hospitali ya
Chake Chake, kuaangalia majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo.
DAKTARI bingwa kutoka Quba anayefanya
kazi zake kisiwani Pemba, (jina halikufahamika) akimtibu mmoja kati ya
majeruhi waliolazwa katika hospitali ya chake chake, kufuatia
kuwangukiwa na ukuta wa mnara wa tangi la Maji Mchomanne Pemba.