
Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya
shughuli zako za kila siku kwa ufanisi. Jambo la kufurahisha ni kuwa
msongo wa mawazi unaepukika, leo nimechambua baadhi ya mambo ambayo
yanaweza kukuwezesha kuepuka kupata msongo wa mawazo.
1. Usiweke Malengo ambayo Hayafikiki
Kila mtu ana uwezo na vipawa vyake tofauti na mtu
mwingine, unapoweka malengo yako hakikisha unazingatia uwezo, vipawa na
muda ulionao ili kuweza kuyafanikisha. Usiweke malengo sababu watu
wengine wameweka hayo,au ukaweka muda kiasi fulani sababu watu wote
wameweka hivyo, daima zingatia uwezo wako ili malengo yako yaweze
kufanikiwa na kuepuka kupata ‘stress’.
2. Jifunze Kukubali Changamoto
Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka
kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila
mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili
changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na
kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu
huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia.
Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.
3. Fanya Maamuzi Pale Unapopaswa
Kutokufanya maamuzi katika muda sahihi hyleta wasiwasi
hofu na msongo wa mawazo. Uwe na ujasiri wa kuamua mara baada ya
kutafakari pande zote kwa makini na kuona faida na hasara za kila
upande. Usihofu sana juu ya kuweza kufanya makosa hadi ukaishia kupata
msongo wa mawazo, mara nyingine watu hujifunza kutokana na makosa.
4. Kuwa na Mipango
Hili nimeshaliongelea sana, angalia hapa . Kutokuwa na mipango ni sababu moja kubwa sana inayoweza kukuletea msongo wa mawazo.
5. Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni
Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni
vyema ukamshirikisha mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu, mume au hata
mshauri. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika
hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya
kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia
kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.
6. Jali Mwili Wako
mara nyingi tunakuwa na shughuli nyingi kiasi cha
kuusahau mwili na kuuchukulia tu kwa juu juu. Ni muhimu sana mwili wako
uwe katika hali nzuri na afya bora ili uweze kufanya kazi zako vizuri na
kwa wepesi. Hakikisha unakula chakula chenye virutubisho bora na pia
unakunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata
muda wa kutosha wa kupumzika kila siku.
Mungu akubariki sana.
Kujirusha kwa raha zako pia husaidia sana katika kuondoa stress, ukiingia club na kujirusha kwa masaa kadhaa kwa raha zako ukitoka hapo roho kwatuuuuu. Namshukuru Mungu sana hii kitu mie naisikia tu namuomba iendelee kuwa hivi.
Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa
kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili.Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya
kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili. Hapa ni baadhi tu ya njia zilizo rahisi ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hali hii pindi unapojikuta umetumbukia ndani yake
1. Jifunze kusema “hapana” hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako… sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.
2.Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, unajua ukikaa chini na kufikiria utagundua kuna mtu flani au kundi flani la watu ndo linalokuleta msongo wa mawazo, sasa kaa nao mbali kabisa.
3. Simamia mazingira yanayokuzunguka. Mazingira yanakuzunguka yanaweza kuwa sababu ya stress zinazokukumba, mazingira yapo nayozungumzia mimi hapa? njia unayotumia kwenda kazini au kurudi nyumbani ina foleni sana? hiyo nayo inawea kuwa sababu ya stress ulizonazo, lakufanya epuka matumizi ya
barabara kwa wakati huo, mazingira ya soko wakati wakufanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali yanakupa stress? nenda katika supermarket maana kwa kiasi flani kuna utulivu na hali ya hewa nzuri
4.Epuka Hasira za haraka, kuna ya mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa
hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka nao ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi
5.Tengeneza orodha ya vitu anavyotaka kufanya sikuhiyo asubuhi tu ukiamka, mara nyingi unapaswa kujua mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni usiwe na viporo, katika orodha
yako tenganisha orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa
mawazo.Naomba niishie hapa kwa leo maana nimewaonjesha yale ninayoyajua na ambayo nimejifunza, swala la kuondoa msongo wa mawazo linapaswa kuangaliwa kiundani zaidi maana ni pana sana, hapa juu nimeongelea
kuepuka stress ambazo si za muhimu ila kuna swala la saikolojia ambalo kwa kadiri siku zinaendelea, tutaligusia.
ninawatakieni afya njema MziziMkavu.