Watafiti wa masuala ya uhusiano na ndoa wana kalenda za
miaka ya hatari iliyotafsiriwa sambamba na sababu zinazoweza kuvuruga
uhusiano na kuwafanya watu waliokuwa wakipendana kuachana.
Hivyo kwa dondoo tu nimeona ni vyema niwafundishe watu wanaoishi kwenye
ndoa sababu zinazotafsiri ukomo wa mapenzi yao kulingana na miaka husika
iliyotafsiliwa na watalaamu wa masuala ya ndoa na uhusiano.
Wanasaikolojia mbalimbali ulimwenguni kupitia tafiti zao walikubali
kuuweka UGOMVI kuwa katika sababu zinazoweza kusababisha ndoa kuvunjika
ndani ya mwaka 1-2. Wanasema endapo watu waliooana wakianza kugombana
kati ya mwezi wa kwanza na kuendelea, basi ujue kuwa wanandoa hao
hawawezi kuvuka miaka miwili kabla ya ndoa yao kuvunjika.
Jambo la kuzingatia katika sababu hiyo ya ugomvi iliyotajwa ni kwamba
watafiti hao hawachukulii hitilafu na migongano ya kawaida kama sababu,
bali mikwaruzano mikubwa yenye kuumiza mwili au roho kwa kiasi kikubwa.
Watafiti hao wanasema wanandoa wapenzi wanaogombana kwa kipindi hicho
huwa na kasoro ya ulinganifu wa tabia, mawazo na mwelekeo hivyo
kuwafanya wasiweze kuishi pamoja kwa muda mrefu.
Hivyo ili wanandoa wasiweze kuachana katika miaka miwili ya mwanzo
wanashauriwa kuoana baada ya kuchunguzana vema tabia na kulingana katika
hali. (Soma TITANIC 1 njia za kuafuta mchumba)
Mwaka mwingine wa hatari ni wa NNE. Baada ya kuoana mwaka wa nne
unatajwa na watafiti kuwa ni wa hatari katika kuwafikisha wapendanao
ukingoni mwa mapenzi yao. Sababu ambayo
inapewa uzito katika kizuizi hiki cha ndoa ni kufanikiwa kupata MTOTO. Kuwekwa kwa mtoto katika kizingiti hiki kunaonekana na tafiti nyingi kuonesha kuwa wanandoa wanapofanikiwa
kupata mtoto hujisahau na kuhamisha mapenzi yao kwa mtoto, huku wakijisahau kuwa wao pia wana jukumu la kupendana.
Watafiti hao wanasema wapendanao wanapokuwa na mtoto, muda mwingi
humfikiria zaidi yeye. Kama ni suala la kuchukua zawadi za kurudi nazo
nyumabani hazitakuwa kwa ajili ya
mume/mke bali itakuwa ni kwa mtoto. Pia msukumo wa kujali, kuhudumia
kubembeleza na ukaribu utahamia kwa mtoto, jambo ambalo litawafanya
wapendanao hao kujiona kama watu wasiohitajiana sana na hivyo kuleta
hatari ya ndoa kufikia ukomo.
Ili kukwepa ndoa kuvunjika katika mwaka huu, wanandoa wanashauriwa kuwa
baada ya kupata mtoto wasisahauliane, wawe na vipindi vya kuwa pamoja na
kushirikiana kamamwanzo, kwa lengo la kulinda upendo wao usiharibike.
Baada ya kuvuka miaka hivyo, mwaka wa saba tangu kuoana unawekwa kuwa ni
mwaka wa kizingiti cha mwisho cha wanandoa kuachana. Kinachosababisha
hatari za mwaka huu kuwemo
katika fungu hilo ni MAISHA, MAJUKUMU NA MAZOEA. Katika kufafanua mwaka huu watafiti hao wameeleza sababu nyingi, lakini za msingi ni hizo ambazo nimezitaja.
Wanasema katika mapito ya maisha kuishi kwa wanandoa ndani ya ndoa kwa
miaka hiyo saba kutakuwa kumewatumbukiza katika kukabili matatizo mengi
ya kimaisha na hivyo kuwafanya
wazidiwe na harakati za kujikimu. Kwanzawatakuwa wamepata majukumu ya
kulea familia, kutunza watoto wao, ambao tayari watakuwa wameanza kusoma
n.k.
Lakini sababu ya kuzoeana inatajwa kuchangia kuondoa msisimko wa
kupendana na hivyo kuamsha hisia potofu kuwa mwanandoa anaweza kuishi
bila mume au mke wake. Hivyo ili kulinda ndoa katika kipindi hiki cha
miaka saba, wanandoa wanashauriwa kutotumia muda wao
mwingi kwenye pilika pilika za kimaisha kiasi cha kukosa muda wa kuwa pamoja.
Hata hivyo wakati watafiti hao wanakubaliana kuwa miaka iliyotajwa ni ya hatari katika
kuvunjika kwa ndoa, bado wanarudi katika kapu hilo kwa kusema wanandoa
ambao wanaachana baada ya kuishi kwa zaidi ya miaka hiyo iliyotajwa,
yaani miaka minane na kuendelea wanaingia katika kundi la wazembe na
wavivu wa kufikiria misingi ya ndoa yao.
Wanasaikolojia wanasema watu walioishi kwa miaka hiyo huwa hawana majibu
sahihi yanayoweza kushibisha sababu za kuachana kwao. Wanachokiamini
wataalamu hao ni kuwa,
hakuna tabia, mwenendo, migongano mabishano na purukushani mpya za
kimaisha zinazoweza kuwatokea wanandoa hao kiasi cha kuonekana kuwa ni
sababu za kupiku mazoea na kushindwa kuvumiliana.
Katika kuhitimisha hilo niseme tu kwamba, ili kuepukana na kikwazo cha
kwanza watarajiwa wa ndoa wanashauriwa kuchanguana kwa kuzingatia
ulinganifu wa tabia. Vijana wengi siku
hizi hawazingatii ulinganifu wa kitabia, badala yake wanachagua wenza
kwa kufuata uzuri na pesa, huku wakilenga kupata sifa toka kwa rafiki
zao
Katika kikwazo cha pili, ushauri uliopo ni kuwa makini juu ya malezi ya
watoto na kuepuka kusahauliana. Watoto wanapaswa kuwa ndani ya upendo
wa mume na mke. Kuhusu kizingiti cha miaka saba, ushauri na kuepuka
kuzoeana na daima kujizatiti kukabiliana na changamoto za kimaisha bila
kukata tamaa. ninawapendeni wote mliop kwenye ndoa ishini vizuri
asanteni.