Mmea wa bangi ukiwa shambani.
TAFITI
mbalimbali zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika masuala ya tiba
duniani, zimethibitisha kuwa mmea aina ya bangi unatibu ugonjwa wa
kansa.
Kwa mujibu wa wataalamu hao kutoka
katika vyuo na taasisi zinazoheshimika duniani, Bangi ilitumika na
inaweza kutumika kutengeneza mafuta ambayo hutibu magonjwa mbalimbali,
ikiwemo kansa ya aina yoyote.
Mbali na kutibu kansa, wataalamu wanasema tayari mmea huo umeonyesha mafanikio katika kutibu magonjwa mengine yapatayo 200.
Miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na
glaucoma, ambao husababisha upofu wa macho, husaidia kuondoa matatizo
yanayojulikana kitabibu kama multiple sclerosis ambayo ni hali ambapo
sehemu mbalimbali ndani ya mwili huwa ngumu. "Bangi
inazui matatizo ya kifafa kwa kiwango kikubwa sana,” alisisitiza Dk.
Robert J. DeLorenzo, Profesa wa Chuo cha kitabibu ya Virginia, nchini
Marekani. Wanasayansi wa Uingereza nao waliwahi kuthibitisha kuwa bangi inaweza kusaidia kuzuia uvimbe unaosababishwa na kansa.
Kumekuwa na harakati za hapa na pale, hususani nchini Marekani na Uingereza za kutaka bangi ihalalish
we na itumike kama tiba.
Hali
hiyo ambayo imekuwa ikizua mvutano ilisababisha wakati fulani Meya wa
Jiji la New York kuunda tume ya wanasayansi kufanya utafiti kuona kama
mmea huo una madhara ambayo yamekuwa yakitajwa, lakini matokeo ya
uchunguzi huo yalibaini kwamba bangi ilikuwa kimea chenye manufaa mengi
kuliko hata bidhaa kama pombe na sigara ambazo ni halali.
"Hakuna
vifo vinavyotokana na matumizi ya bangi. Hakuna popote pale," alisema
Dk. Lester Grinspoon, Profesa wa Chuo cha kitabibu cha Harvard.
"Sijawahi
kusikia mtu kavuta kete kumi za bangi na akafa kwa ajili ya kuzidi
vipimo, ila nimewahi kusikia na kuona mtu kameza vidoge vya malariquin
ama madawa haya vya kisasa na kufa kwa ajili ya kuzidi vipimo vya dawa,”
alisema Dk. Paul Hornby, mwana biolojia na mkemia (biochemist) pamoja
na kuwa pathologia wa binadamu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini
katika utafiti wa bangi.
Majarida
mbalimbali yaliyochapishwa na wanasayansi kutoka katika vyuo vya
kitabibu kama Harvard yanaeleza kwamba bangi ni muhimu katika afya ya
binadamu, na inaweza kutibu matatizo ya binadamu kuliko madawa
yanayopikwa kwenye maabara.
Marehemu
Dk. Tod Mikuriya, aliyekuwa mtawala katika serikali ya Marekani katika
utafiti wa bangi, alisema kwamba baada ya kushugulika na madawa
mbalimbali karibia elfu kumi, bangi ilifanya vizuri zaidi katika
magonjwa mbalimbali kama 200.
Pamoja
na kwamba bangi hairuhusiwi kisheria hapa nchini, hata hivyo kwa miaka
mingi katika nchi za wenzetu imekuwa ikitambulika na kutumika katika
kutibu magonjwa fulani fulani.
Mbali
na kuonekana kuwa na mafanikio na katika magonjwa hayo, pia nchini
Marekani na nyingine za bara la Ulaya imekuwa ikitumiwa kuongeza nguvu
katika tiba ya wagonjwa wa Ukimwi.



