
Takwimu
zinaonyesha kuwa watu wanaougua ugonjwa huo wameongezeka kutoka 10,286 katika
kipindi cha waka 2011 hadi kufikia 15,838 mwaka 2012.
Hayo
yalibainishwa jana na kaimu mratibu wa magonjwa ya akili mkoani Kilimanjaro Bi.
Ester Maro, wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake kuhusiana na hali ya
ugonjwa huo na jitihada ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali katika
kukabiliana na tatizo hilo.
Bi.
Maro ambaye ni afisa muuguzi kitengo cha magonjwa ya akili katika hospitali ya mkoa wa
Kilimanjaro Mawenzi, alisema pamoja na ugonjwa huo kuwatesa wananchi wengi, dawa
bado ni tatizo kubwa ambalo linakwamisha jitihada za mkoa za kumaliza tatizo
hilo.
“Hali
ya magonjwa ya akili katika mkoa huu bado si ya kuridhisha,na wagonjwa wanaougua
ugonjwa huu wamekuwa wakiongezeka kwa kasi sana kila kukicha,lakini pamoja na
tatizo hili kuendelea kuwa kubwa upatikanaji wa dawa umekuwa wa shida sana hali
ambayo imekuwa ikiwafanya wananchi wengi hasa wa kipato cha chini kukata tama
kutokana na kukosa fedha za kununua dawa hizo kwenye maduka ya dawa ya
binafsi”alisema Bi. Maro.
Aidha
alisema kukosekana kwa dawa kwenye hospitali kunatokana na bohari ya dawa MSD
nayo kukosa dawa hizo hali ambayo imekuwa ikiwafanya madaktari na wauguzi katika
vitengo vya magonjwa ya akili kuwaagiza wagonjwa kwenda kununua dawa kwenye
maduka ya dawa.
“Dawa
za magonjwa ya akili zinauzwa kwa gharama kubwa katika maduka ya dawa,hali hii
huwakwaza wagonjwa wengi na kuwafanya waache kutumia dawa na kuishia
mitaani,lakini pia tatizo hili la ukosefu wa dawa limezifanya familia nyingi
kuwatenga wagonjwa wa akili kwa kuona hawawezi kuwahudumia hivyo kuishia kuishi
mitaani na kula majalalani”alisema
Kutokana
na hali hiyo Bi. Maro aliishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza bajeti
ya dawa ili kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa kero na kikwazo kikubwa kwa
wagonjwa.
Akizungumza
na TAIFA LETU.com, mganga
mfawidhi
wa Hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi
Dkt.Saganda Kapalala alikiri
kuwepo kwa tatizo kubwa la ukosefu wa dawa za magonjwa ya akili na kusema kuwa
hali hiyo imekuwa ikiwasumbua na kuwaumiza kichwa madaktari na wauguzi wa
kitengo hicho.
Alisema
kutokana na tatizo hilo Hospitali imekuwa ikijitahidi kununua dawa zamagonjwa
hayo ili kupunguza tatizo na kuwasaidia wagonjwa ambao wengi wao hawamudu
gharama za dawa.
“Tatizo
la dawa za magonjwa ya akili linaninyima usingizi,kwani limekuwa tatizo kubwa na
wagonjwa wanapofika hospitali na kuagizwa wakanunue dawa huwa wanaona kama
wanaonewa kutokana na kwamba hospitali dawa hizi huwa zinatolewa bure,niwaombe
MSD wajitahidi kuagiza dawa hizi ili kutupunguzia mzigo na
tatizo”alisema