Pichani kati
ni Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando akizungumza mbele ya
Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala
jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku
ya Mama Duniani itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo
kauli mbiu ya Mwaka huu imepangwa kuwa ni "always in our heart's",
"tukiwakumbusha akina mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda
sana" alisema Chando.Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa
na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo,Bi.Regina Ogwalla.Bahati amesema kuwa
katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT
Ilala,Mh.Nora Mzeru.
Miss Earth
Tanzania 2012,Bahati Chando amesema kuwa ameamua kuungana na Diwani wa
kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo itakayozinduliwa na
Wamama wa Ilala,kutambua umuhimu wa kina mama,kuwafurahisha lakini pia
kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku
kubwa ya kuandaa sherehe kama hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama
watu wengi walivyoungana kumsaidia katika safari yake ya kuwa mrembo wa
kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.
Pia anasema
kuwa ameandaa sherehe hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au miss
sio tu kupozi mbele ya Kamera,bali inaambatana na na jukumu la kugusa
jamii kwa namna mbalimbali.
Shoto ni
Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa akitoa ufafanuzi kuhusiana
na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama
Duniani itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu
ya Mwaka huu kwenye hafla hiyo umepangwa kuwa ni "always in our
heart's",