Blogger Widgets

Social Icons

Pages

Monday, April 29, 2013

Wema Sepetu kuigiza kwenye filamu na staa mkubwa wa Nigeria, usaili wa waigizaji wengine kufanyika May 4

Hivi karibuni staa wa filamu nchini Wema Sepetu anatarajia kuigiza kwenye filamu moja na staa wa mkubwa wa Nigeria ambaye hata hivyo kwa mujibu wa kampuni inayosimamia filamu hiyo, jina lake bado ni siri.
389749_122116034595413_1233322461_n

Kampuni ya Rimacy Entertainment Group ya Tanzania ndio itakayoifanya filamu hiyo. Kwa mujibu wa mratibu wa mchakato huo Seif Kabelele filamu hiyo ambayo jina lake bado halijawekwa wazi, itazinduliwa Tanzania, Kenya, Uganda, Uingereza na Marekani.
Amesema May 4 kutafanyika usaili wa waigizaji wengine zaidi ya watano watakaoukula shavu kwenye filamu hiyo.
Usaili utafanyika Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Huu ni mchanganuo wa waigizaji wanaohitajika:
•A Girl / 5-8 Years. / Any Ethnicity
•Female / 25-30 Years. / Any Ethnicity
•Male/ 31-40 Years. / Any Ethnicity
•Male / 41-50 Years. / Caucasian
•Male / 18-24 Years. / Any Ethnicity
•Female / 18-24 Years. / Any Ethnicity
•Male / 25-30 Years. / Any Ethnicity
•Female / 25-30 Years. / Caucasian
•Male / 31-40 Years. / Any Ethnicity
•Female / 31-40 Years. / Any Ethnicity
.Female / 51-60 Years./ Any Ethnicity
.Male / 31-40 Years./ Caucasian
Kwa maswali wasiliana na email hii: rimacy.group@yahoo.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...