
Msaniii
wa Miondoko ya Hip Hop Roma Mkatoliki akitoa burudani kwa maelfu ya
wakazi wa Mwanza waliofurika katika viwanja vya Furahisha mkoani humo
kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha uliofanyika
mwishoni mwa wiki kwa siku mbili mfululizo.
Msanii
wa Bongo Flava toka kundi la Tip Top Connection lenye makazi yake mtaa
wa Manzese Dar es Salaam maarufu kwa jina la Madee akitumbuiza katika
tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha
lililofanyika mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha mwishoni mwa
wiki hii.
Msanii
wa Hip Hop anayeshabikiwa kwa wingi, Nay Wamitego, akikamua wakati wa
tamasha maalum la uzinduzi wa Airtel Yatosha mkoani Mwanza katika
viwanja vya Furahisha.
Msanii
Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani mashairi
yenye mvuto kwa miondoko ya Hip Hop wa mkoani Mwanza maarufu kwa jina la
Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la Airtel Yatosha
mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha.
Wananchi mbalimbali wa mkoani Mwanza walijitokeza na kujiuga na Airtel ili waweze kutumia huduma za Airtel Yatosha.
---
WASANII BONGO FLEVA WAFUNIKA KAMPENI YA AIRTEL YATOSHA JIJINI MWANZA
WASANII wa
muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) wamefunika kwa kutoa burudani ya
nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel nchini ya airtel
yatosha na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki huo waliofurika
katika viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.
Kampeni
hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na kushuhudia na
maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa Airtel yatosha
kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na jinsi ya kutumia
huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata dakika nyingi za
muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei nafuu zaidi kwa laini
moja tu ya Airtel.
Wasanii wa
Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi maelfu ya wananchi
waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye vituo mbalimbali vya
redio na televisheni hapa nchini ni pamoja na Juma Khasim ‘Nature’ na
kundi lake la wanaume halisi, Roma Mkatoliki, Madee na Ney wa Mitego.
Maelfu ya
wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia kushuhudia vipaji vya
uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na waliojitokeza kucheza
muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na kupata zawadi ya laini na
fulana (T-shirt) za Kampuni ya Airtel zilizotolewa kwa washindi
waliopatikana.
“Wananchi
wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa
muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea lakini pia wengi kwa sasa
wanatumia mtandao wa Airtel ikiwemo huduma hii ya Airtel yatosha pamoja
na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya kutumia huduma
hii”alisema msanii Ney wa Mitego.
Akizungumzia
Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson Mmbando alisema
kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika katika mikoa sita hadi sasa hapa
nchini kumekuwa na mapokeo na mafanikio makubwa kwa kuongeza wateja
wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma zote.
Mfanyabiashara
wa vituo vya kuuza mafuta Barnabas Mathayo wa Jijini Mwanza alitoa
ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel katika mahojiano
maalumu alisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya Airtel yatosha
amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda wa kutosha
kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanao nunua
mafuta kwaajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kupitia mitandao yote kwa bei ile ile.
“Huu ni
Mkoa wa sita sasa na kama mlivyoshuhudia wingi wa watu wanaokuja
kushuhudia burudani na kupata maelezo ya jinsi ya kutumia mtandao huu
kwa garama nafuu zaidi na ikizingatiwa Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa
inayojishugulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji na wafanyabiashara kutoka
ndani na nchi za maziwa makuu”alisema Meneja huyo.
“Hatukaangi
laini ni moja tu yatosha zingine za nini na ukiangalia Mwanza ni Mkoa
wa burudani, biashara, viwanda, kilimo, uvuvi na ufugaji hivyo wananchi
wake hawana budi kutumia mtandao wa Airtel ambao umedhamiria kuwainua
kiuchumi na kuletwa kwa kampeni hii itawasaidia kujifunza Airtel kuna
nini ndani ya mtandao huu”alisema Mbando aliongeza kuwa kampeni hiyo
inaendelea katika Mikoa ningine na mwishoni mwa juma hili kampeni hiyo
itahamia Jiji kubwa la Dar es salaam katika viwanja vya Zakhem na
kutakuwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali
kutokana na wasanii wengi kuwa
jijini
humo na kutoa wito kwa wananchi kufika kushuhudia na kujifunza ndani ya
mtandao wa Airtel kuna vitu gani na kwa gharama nafuuu.



