Mzozo wa
eneo tengefu la pori la Loliondo Wilayani Ngorongoro katika Mkoa wa
Manyara, sasa limetua kwa Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupata
ufumbuzi. Siku
za karibuni, mzozo kati ya wakazi wa eneo hilo na Serikali uliibuka
baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
kutangaza Serikali kuchukua ekari 1,500 na kuwaachia wakazi wa eneo hilo
kumiliki ekari 2,500 hatua waliyoikataa.
Katika
mikutano yake na waandishi wa habari mwishoni mwa Machi na mwanzoni mwa
mwezi huu, Waziri Kagasheki alishikilia msimamo wa Serikali kuwa uamuzi
uliotolewa na wizara yake ni sahihi na hautabadilika.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Elias Ngolisa akitoa taarifa ya
mkutano wao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mkutano wa hadhara
uliofanyika juzi, Kijiji cha Arash, wilayani Ngorongoro, alisema baada
ya kutoa maelezo yao na vielelezo, Waziri Mkuu aliahidi kupeleka mgogoro
wao kwa Rais Kikwete kwa kwa ajili ya kutolea uamuzi.
“Kama
ambavyo mlitutuma, tulikutana na waziri mkuu na viongozi wengine,
ikiwepo Tume ya CCM na tumemweleza waziri mkuu kwa nini tunapinga agizo
la Waziri Kagasheki.
Habari na Mussa Juma, Mwananchi
Chanzo - Mwananchi



