MTUHUMIWA
wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten
mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari wa FFU mwenye namba G2573
Pasificus Cleophace Simoni (23)akwama kufikishwa mahakamani baada ya
kudaiwa kuwa ni mgonjwa.
Mtuhumiwa huyo alipaswa kufikishwa mahakamani hapo jana ila hakufikishwa kabisa.
Mbali ya
watu mbali mbali kufika katika Mahakama hiyo ya hakimu mkazi mkoa wa
Iringa kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo bado mahakama hiyo ilielezwa
kuwa mtuhumiwa huyo ameshindwa kufika mahakamani leo kutokana na tatizo
la ugonjwa linalomsumbua ambapo hata hivyo haijaelezwa mtuhumiwa huyo
ana sumbuliwa na nini.
Kutokana
na mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na ugonjwa hakimu wa
mahakama hiyo Mary Senapee alihirisha kesi hiyo hadi Mei 9 itakapofika
mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa tena.
Kesi hiyo
yenye mvuto mkubwa kwa wakazi wa mkoa wa Iringa na watanzania pamoja na
dunia kwa ujumla imekuwa ikiendelea kutajwa katika mahakama ya hakimu
mkazi mkoa wa Iringa na hadi sasa ni zaidi ya mara 12 imekuwa ikitajwa
bila kusikilizwea .