Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya
maua kutoka kwa watoto wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la
Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya
kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo
iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya
Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza
na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto
wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika Kituo
cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, leo kwa ajili ya
kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo
iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya
Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza
na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto
wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya
kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la
Msasani, Joseph Mayala, leo wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia
ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya
kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International
Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam
na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo. Kulia
ni Askofu wa Kanisa hilo, Dkt. Mathew Byamungu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini
wa dini ya Kikristo wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la
Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya
kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo
iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya
Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza
na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto
wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
Baadhi ya waumini waliohudhuria harambee hiyo.
Watoto wa Kwaya inayofadhiliwa na
Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani ya kuimba
moja ya wimbo wao ulio katika Albam yao iliyozinduliwa katika hafla
hiyo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Dkt. Mathew Byamungu, akitoa neno la shukrani baada ya hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja ya kumbukumbu na watoto wanaounda kundi la Kwaya ya watoto,
inayofadhiliwa na Shirika hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja ya kumbukumbu na Watoto wa Kituo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wachungaji na watumishi wa Kanisa
hilo.