Kada wa chadema atiwa mbaroni kwa kosa la kummwagia tindikali ndugu musa wakati wa uchaguzi wa Igunga
MUSA TESHA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI
Kada
maarufu wa CHADEMA Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,Jumamosi
alikamatwa na askari polisi na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu
alisafirishwa kwenda Tabora na kukabidhiwa kwa askari wa huko. Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa
Tesha 9 Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa
Mbunge ambapo mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa
CHADEMA bwana Joseph Kashinde.
Bwana Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana na askari nane ambao hawakuvaa sare.
Baada ya mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee ili wawe mashuhuda wakati wanampekua.
Hata hivyo,polisi hao hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na
kuamua kuondoka naye kwenda kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia
hawakuambulia kitu.
Taarifa iliyopatikana jana mchana kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda kutibiwa.